24
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Kumi na Tatu: KUSOMA KWA UFASAHA Moduli ya Mwalimu

Moduli ya Mwalimu - tie.go.tztie.go.tz/docs/MODULI YA MWALIMU-KUSOMA KWA UFASAHA.pdfKaratasi ya bodi ya hadithi ambayo ulikamilisha ... mara ya kwanza, soma sentensi kwa shauku na

Embed Size (px)

Citation preview

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III

Moduli ya Kumi na Tatu: KUSOMA KWA UFASAHA

Moduli ya Mwalimu

1Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiOfisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu TanzaniaChuo Kikuu cha Dodoma

Chuo cha Ualimu MorogoroChuo Kikuu cha Dar Es SalaamChuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu MkwawaEQUIP-Tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U ButimbaC.C.U Bustani C.C.U Tabora C.C.U Ndala C.C.U Kasulu

C.C.U Kabanga C.C.U BundaC.C.U Tarime

C.C.U ShinyangaC.C.U Mpwapwa

2 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Namna ya kutumia moduli ya mwalimuModuli hii ina vipengele vifuatavyo katika kuifanya iwe rafiki kwa mwalimu: 1) Maudhui ya Moduli; 2) Dhana Kuu; 3) Malengo ya Moduli; 4) Maelekezo Muhimu kuhusu Moduli; 5) Taratibu za kujifunza kwa kila kipindi cha mafunzo.

Moduli hii imekusudiwa kutoa fursa kwa mwalimu kusoma na kujifunza kwa vitendo kwa kushirikiana na walimu wenzake pamoja na Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule. Baada ya kila kipindi cha mafunzo, mwalimu anategemewa kutumia mikakati ya ufundishaji na kujifunza darasani kwa lengo la kujenga umahiri wa mwanafunzi wa kusoma. Aidha, moduli hii inatoa maelekezo yaliyo ya wazi na yenye kufuata hatua kwa hatua katika uandaaji wa zana za kufundishia na kujifunzia stadi za kusoma na kuandika.

Moduli hii ina kipengele cha ufuatiliaji na tathmini ambacho hutoa nafasi kwa mwalimu kutoa mrejesho kuhusu dhana na maudhui ya moduli, uwasilishaji wa Mratibu wa Mafunzo ya Mwalimu Kazini na ushiriki wa walimu wakati wa mafunzo kwa lengo la kuboresha mafunzo ya walimu kazini ngazi ya shule.

3Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO NA TASWIRA KATIKA MODULI

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Zifuatazo ni mifano ya taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu mwalimu anafanya kazi na mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika fikra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya KUFUNDISHA wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.

4 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MODULI YA 13: KUSOMA KWA UFASAHA

MAUDHUI YA MODULIModuli ya 5 – 8 inahusu dhana na mbinu za KUFUNDISHA kusoma ambazo zinaendana na mabadiliko yaliyo kwenye muhtasari mpya wa darasa la kwanza na la pili. Moduli hii pia inahusu baadhi ya dhana na shughuli kama zilivyoanishwa kwenye muhtasari mpya wa darasa la kwanza na la pili. Moduli hii inahusu ufasaha, au kusoma kwa kasi inayohitajika, usahihi na kwa hisia. Kwa ujumla hii inamaanisha kwamba wanafunzi wanasoma kama wanaongea tu – wanasoma ili msikilizaji aelewe na wanasoma kwa hisia kufanya matini ivutie. Ufasaha unaendana na umahiri wa kusoma. Kuwa na ujuzi wa kusoma kwa ufasaha kunamaanisha kuwa wanafunzi wanaweza kuelewa vizuri na kufurahia wanachokisoma.

DHANA KUU1. Kasi – Idadi ya maneno ambayo msomaji anaweza kusoma kwa muda maalum (Kwa mfano. Maneno

48 kwa dakika) 2. Usahihi – Usomaji usio na makosa. Je msomaji anafanya makosa?3. Hisia– Kusoma kwa lafudhi na kwa kuzingatia alama za uandishi ili kusaidia kubeba maana ya matini.4. Maneno ya kawaida – Maneno ambayo wanafunzi wanayafahamu kwa sababu wanayatumia mara nyingi

katika kuongea na kuandika bila hata ya kufundishwa, Kama vile“kwa”, “na”, “ni” .5. Alama za uandishi – Alama zinazotawala utiririkaji na uelezaji wa sentensi. Mifano inajumuisha, alama ya

mshangao, alama ya kuuliza, alama ya kituo kikuu, kituo kidogo na alama ya kunukuu.

MALENGO YA MODULIMwisho wa moduli hii, wanafunzi watakuwa na uwezo wa:1. Kuelewa kwa nini kusoma kwa kasi, usahihi na hisia vinaendana na kusoma kwa ufasaha2. Kuelewa mbinu ambazo zinajenga uwezo wa mwanafunzi katika kusoma kwa kasi, usahihi na hisia3. Kutumia mbinu hizi kuimarisha ujuzi wa ufahamu wa kusoma darasani4. Kutengeneza kitabu kikubwa ili kusaidia mbinu mbalimbali za kusoma

MAELEKEZO MUHIMU Njoo na vitu vifuatavyo:1. Moduli ya mafunzo ya walimu kazini na kalamu2. Karatasi 3 – 5 za A23. Penseli4. Karatasi ya bodi ya hadithi ambayo ulikamilisha katika kipindi kilichopita5. Viweka alama na rangi6. Mkasi7. Kamba

TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama

inavyoonekana katika picha.2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki

wote waonane na kuongea kwa pamoja.3. Waeleze walimu wawe huru kuuliza maswali

kama hawajaelewa.4. Waeleze walimu kuwa msaada kwa wenzao.5. Waeleze walimu kuwa wabunifu na kufikiria dhana

watakazojifunza na jinsi zitavyohusiana na darasa lao.6. Waeleze walimu waweke simu zao katika hali

ya mtetemo.

5Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAFAKARI

Katika kipindi cha mwisho tulisoma kuhusu kusoma kwa ufahamu. Orodhesha mafanikio uliyoyaona pamoja na changamoto ulizokabiliana nazo wakati wa KUFUNDISHA maudhui ya moduli hiyo darasani kwako.

ANDIKA PEKE YAKO (DAKIKA 5) Tafadhali andika kwenye visanduku mafanikio na changamoto ulizokutana nazo wakati wa kutekeleza mikakati hii katika darasa lako.

JADILIANA KATIKA KIKUNDI (DAKIKA 10)1. Shirikisha wenzako kwenye kundi mojawapo kuhusu uzoefu huo. 2. Kwa kila changamoto, pendekeza namna ya kukabiliana nayo.3. Wakati wa majadiliano, andika ufumbuzi unaoendana na changamoto ulizobainisha.

Mafanikio(Elezea utaratibu uliotumia na fafanua jinsi ulivyofanikiwa)

Changamoto (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua changamoto zake)

Njia Muhimu za Ufumbuzi(Mawazo muhimu na mahususi kwa wenzetu)

6 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

ZOEZI LA KUCHANGAMSHA (DAKIKA 10) Leo, tutaanza na shughuli ya kusoma. Walimu mtasoma kwa kufuata maelekezo.

1. Baada ya kusoma sentensi hiyo hapo chini, pigia mstari maneno ambayo unafikiri hayafahamiki kwa wanafunzi wako. Haya ni maneno ambayo watahitaji kuyahusianisha ili kuyasoma kwa sauti. (Kumbuka, kuhusianisha ni wakati unafasiri neno kutoka kwenye maandishi kuwa matamshi, kwa kuvunja neno katika sauti moja moja (Kutenganisha fonimu) na kuunganisha sauti ili kutamka neno (Kuunganisha fonimu).

2. Kisha zungushia maneno ambayo unafikiri wanafunzi wanaweza kuyatambua haraka kwa kuyaangalia (na watahitaji kuyahusianisha).

3. Baada ya kuzungushia na kupigia mstari maneno, kila mwalimu ageuke na kusoma sentensi kwa sauti kwenye kundi. Kila mtu asome sentensi mara mbili: mara ya kwanza, soma sentensi kwa shauku na msisimko. Mara ya pili, soma bila kusimama mwishoni mwa sentensi na bila kuonyesha hisia.

FIKIRI – WAWILIWAWILI - SHIRIKISHA Baada ya mratibu kusoma maneno yote, jadili maswali yafuatayo hapa chini pamoja na mwenzako:

1. Maneno gani ulipigia mstari kwa sababu ulifikiri hayafahamiki kwa wanafunzi wako?

2. Maneno gani ulizungushia kwa sababu ulifikiri wanafunzi wako wanaweza kuyajua na kuyatambua mara moja?

3. Unadhani ina maana gani mtu anasoma bila kusimama na bila hisia?4. Unadhani ina maana gani mtu anasoma matini kwa hisia?

Mama akarudi nyumbani. Mtoto wake akamkimbilia na akasema, “Mama! Kuna moto ndani!”

7Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Katika zoezi la kuchangamsha, uligusia ujuzi wa aina tatu ambao unaendana na kusoma kwa ufasaha: kasi, usahihi na kujieleza. Wakati mwingine tunasema kusoma kwa ufasaha ni “kusoma kama vile unaongea,” kwa sababu kusoma kwa kasi inayotakiwa, kwa usahihi, na kwa hisia kunahakikisha kuwa msikilizaji anakuelewa kiasi cha kutosha. Kusoma kwa ufasaha pia kunaonesha kwamba wanafunzi wamefikia kiwango cha juu cha umahiri katika foniki, msamiati na ufahamu.

KasiWasomaji wapya mara nyingi husimama na kuanza wakati wanasoma ili kuhusianisha maneno wasiyoyafahamu. Kuhusianisha ni muhimu na ni kitu kizuri kufanya, lakini wakati mwanafunzi anasoma polepole sana, hawezi kukumbuka nini alichosoma mwanzoni mwa sentensi wakati ambapo atakuwa mwisho wa sentensi. Hii inafanya kuwe na ugumu katika kuelewa ujumbe ambao sentensi inajaribu kuufikisha. Maneno ambayo unazungushia kwenye zoezi la kuchangamsha ni mifano ya maneno yasiyofahamika ambayo yatapunguza kasi ya mwanafunzi kwa sababu anahitaji kuhusianisha. Kwa hiyo, wanafunzi wanapaswa kufanya mazoezi ya kuhusianisha haraka ili waweze kusoma kwa kasi ya uongeaji.

Namna nyingine ya kukuza kasi katika usomaji wa wanafunzi ni kukuza idadi ya maneno ya kawaida ambayo wanayafahamu. Maneno ya kawaida ni maneno ambayo yanatokea mara nyingi katika matini zinazosomwa au zilizoandikwa, kama vile “kwa”, “na”, “mama”, “baba”, na “kula”. Wanafunzi lazima watambue maneno haya bila kuyahusianisha. Hii itawasaidia kusoma kwa kasi inayohitajika bila kuwa na kazi ya kujishughulisha na kila neno moja liliko kwenye ukurasa.

Kwa hiyo, kasi ya wanafunzi katika usomaji itaongezeka kama watakuwa na uwezo wa kutambua maneno machache moja kwa moja, halafu wakahusianisha maneno yaliyobakia haraka. Kwa mfano, kutegemeana na ngazi ipi unafundisha, sentensi yako kutoka kwenye zoezi la kuchangamsha inaweza kuonekana kama hii hapa chini. Kazi ya mwalimu ni kuongeza idadi ya maneno ya kawaida ambayo wanafunzi wanayafahamu, na pia kuwasaidia wahusianishe maneno wasiyoyafahamu haraka zaidi.

UMUHIMU WA KUSOMA KWA UFASAHA (DAKIKA 35)

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha sehemu (kwa mfano, aya au maelezo) amwite mwalimu mwingine kwa jina asome sehemu inayofuata.

2. Wakati unaposoma zingatia alama zifuatazo: • Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu.• Weka alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo.• Weka mduara katika (o) maneno ambayo ni mapya.

MIFANO YA MANENO YA KAWAIDA KATIKA KISWAHILI

kwana

mama

babakula

mtoto

dadapika

sema

somaonalala

8 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Mama akarudi nyumbani. Mtoto wake akamkimbilia na akasema, “Mama! Kuna moto ndani!”

Mbinu za kujenga kasi:

1. Kuza ujuzi wa kuhusianisha – Rudia shughuli katika moduli ya 8 kama “jina – neno kuu – sauti” na “chapa herufi” kuimarisha uwezo wa wanafunzi kuoanisha sauti herufi na herufi zilizoandikwa mara moja. Pia, rudia mbinu za kuimarisha ujuzi wa kuhusianisha na kuunganisha kutoka moduli ya 9 kama vile kutumia kadi herufi, “silabi za siri” na “kuoanisha silabi”, fanya hivyo pamoja na darasa.

2. Kuza /Ongeza maarifa ya maneno ya kawaida – Wanafunzi tayari wanafahamu maneno mengi ya kawaida kwa sababu ya kuyarudia mara nyingi kwenye Kiswahili kinachoongewa au kuandikwa. Japokuwa, unaweza kukuza idadi ya maneno ya kawaida ambayo wanafunzi wanayafahamu kwa kutengeneza kadi za maneno na kuzitundika kwenye ukuta wa maneno ili wanafunzi wazione na kuzisoma muda wowote.

3. Onesha kasi inayotakiwa katika kusoma ambayo inasaidia ufahamu – Wanafunzi wanajifunza kwa kuangalia viongozi wa mifanowalimu wao. Ukisoma kwa kasi ambayo inawafanya wao waelewe matini, wataiga kasi hiyo. Shughuli ya kwanza katika sehemu ya Mpango Kazi itakusaidia kulifanya hili.

Usahihi

Wanaosoma kwa usahihi husoma karibia maneno yote katika matini . Njia moja ya kuwasaidia wanafunzi kukuza usahihi wao katika kusoma ni kuimarisha msamiati wao na kwa kufanya mazoezi ya kuhusianisha. Kama unakumbuka, msamiati wa wanafunzi unahusisha maneno ambayo wanafunzi wanayatambua mara moja na kufahamu maana yake. Hii pia inaweza kujumuisha maneno ya kawaida. Kama ilivyojadiliwa mapema, kuweka neno jipya kwenye ukuta wa maneno kunakuza uelewa wa wanafunzi kuhusu maneno hayo ili wayatambue wakikutana nayo katika muktadha mwingine. Hakikisha kwamba wanafunzi wanakumbuka maana yake na namna ya kuyatamka kwa usahihi.

Siku zote kutakuwa na maneno mapya ambayo wanafunzi hawataweza kuyaelewa papo kwa papo, ikiwa wanafunzi wanaweza kutambua kwa usahihi sauti herufi ambazo zinahusiana na maneno yanayoandikwa katika maneno haya mapya, watakuwa na uwezo wa kuhusianisha na kutamka neno kwa usahihi.

Maneno ya kawaida ambayo wanafunzi wanapaswa kuyafahamu moja kwa moja.

Maneno Mapya au yasiyofahamika (kutegemeana na ngazi ya kusoma) ambayo wanafunzi wanahitaji kuhusianisha.

9Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Mbinu za kujenga Usahihi:

1. Kuza ujuzi wa kuhusianisha – Kwa kuongezea mbinu zilizoorodheshwa kwa ajili ya kasi, kwa kawaida wasomaji wanaohusianisha (mmoja mmoja au pamoja na mwenzako pia wanawapatia wanafunzi mazoezi ya ziada katika kuhusianisha na kuunganisha. Kama umepokea vitabu vya ziada kutoka EQUIP-Tanzania, vitabu vya ‘Tusome’ ni vizuri kwa wanafunzi kufanya mazoezi ya kuhusianisha.

2. Kuza maarifa ya maneno ya kawaida – Kwa kuongezea kwenye mbinu zilizoorodheshwa kwa ajili ya kasi, hakikisha mara kwa mara unarejea na kupitia maneno kwenye ukuta neno wako. Hakikisha wanafunzi wanakumbuka maana zinazoambatana na maneno yaliyochapishwa.

Kiimbo

Wasoma kwa ufasaha pia wanasoma kwa hisia inavyotakiwa. Wanatumia alama za uandishi kujua wapi watulie wakati wanasoma na wapi waweke msisitizo kwenye baadhi ya maneno. Wasoma kwa ufasaha wanaelewa maana ya matini wakati wanasoma ili wasome kwa hisia. Katika zoezi la kuchangamsha, ulitoa mifano ya kusoma bila kujieleza (bila kutulia au kusisimua) na kusoma kwa kujieleza na shauku (ambavyo viliwezekana kutokana na uelewa wako wa alama za uandishi na ufahamu wako wa msamiati).

KUFUNDISHA alama za uandishi kutakuza kusoma kwa hisia kwa wanafunzi, na ni muhimu kwamba wanafunzi wako waelewe kwamba alama za uandishi zinawapa maelekezo ya namna ya kusoma sentensi. Kwa mfano:

1. Kituo kidogo () inaonesha kwamba unapaswa kutulia kidogo katika sentensi. 2. Kituo kikuu (.) kinaonesha kwamba sentensi imefika mwisho na unapaswa kutulia kwa muda

mrefu zaidi.3. Alama ya mshangao ( ! ) inaonesha kwamba sentensi imefika mwisho, lakini unapaswa kuimalizia

kwa shauku 4. Alama ya kuuliza (?)Inaonesha kwamba, sentensi imefika mwisho, lakini ni swali .Hivyo usikikaji wa

sauti yako lazima uongezeke, kama vile unauliza swali.5. Alama za kunukuu (“”) inaonesha kwamba unapaswa kusoma maneno yaliyoko katika nukuu kwa

msisitizo.

Kwa darasa la 1 na 2 walimu wapaswa KUFUNDISHA kituo kidogo, kituo kikuu and alama ya kuuliza. Baa-da ya kueleza maelekezo haya, itasaidia kuwaonesha wanafunzi mifano ya alama hizi za uandishi katika matini. Kisha soma matini kwa sauti weka msisitizo kwa vitendo kama ilivyooneshwa na alama za uandishi husika, na baaadaye watake wanafunzi wafanye kama ulivyofanya. Pia, unaweza kucheza mchezo na wanafunzi (kwa kutumia kadi za alama za uandishi ambazo ulizitengeneza wakati wa moduli ya 8 ya kuimarisha uelewa wao juu ya maelekezo haya:

10 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Mbinu za kujenga uwezo wa kujieleza:

1. Fundisha alama za uandishi – Shiriki mchezo huo hapo juu pamoja na wanafunzi. Na hakikisha kila unapoandika sentensi kwenye ubao, mara zote tumia alama za uandishi. Hakikisha unawakumbusha wanafunzi kitendo gani alama hizo zinawakilisha.

2. Kukuza msamiati na ufahamu – Wanafunzi wanapoelewa matini, wanakuwa katika nafasi nzuri ya kubaini ni aina gani ya hisia wanazopaswa kutumia. Rudia mbinu KUFUNDISHA na kufanya mazoezi ya msamiati mpya (Moduli ya 11), na mara zote tumia maswali ya “kabla, wakati na baada” kukuza ufahamu (Moduli ya 12).

3. Waoneshe wanafunzi kusoma kwa hisia kunakotakiwa – Kama ilivyo kwenye kuonesha kasi inayotakiwa, wanafunzi wanaweza kujifunza kujieleza kunakotakiwa kwa kukuangalia ukisoma kwa sauti na kwa kujieleza. Mwongozo wa somo la kwanza kwenye sehemu ya mpango kazi inaonesha namna moja ya kulifanya hili.

Mchezo wa alama za uandishi:

Omba watu wawili wanaojitolea wasimame nyuma ya darasa wakati wewe umesimama mbele ya darasa. Waambie watembee polepole kutokea nyuma ya darasa kuja mbele, wakati wakitembea utashikilia kadi tofauti za alama za uandishi. Kwa kila kadi, wanafunzi lazima wafanye kitendo kinachoendana na jambo ambalo alama zinawakilisha. Kwa mfano:

1. Mkato (,) inaonesha kwamba wanafunzi lazima watulie na kisha waendelee kutembea. 2. Kituo kikuu ( . ) inaonesha kuwa wanafunzi lazima waache kutembea hadi utakapowaelekeza

kuendelea tena3. Alama ya mshangao ( ! ) inaonesha kuwa wanafunzi wanapaswa kuacha kutembea kisha

waruke juu kwa shauku4. Alama ya kuuliza ( ? ) inaonesha kuwa wanafunzi lazima waache kutembea na kisha

wanyooshe mikono yao hewani kujaribu kugusa dari5. Alama ya kunukuu (““ ) inaonesha kuwa wanafunzi wapunge mikono yao hewani wakati

wanatembea.

Kama una darasa kubwa, unaweza kushikilia kadi kadhaa wakati wanafuzi wanatembea kutoka nyuma kuja mbele ya darasa. Wafafanulie wanafunzi kwamba mchezo huu ni sawa na wakati mtu anasoma. Wanafunzi wakishatembea, wanapaswa kufuata vitendo ambavyo alama za uandishi zinawakilisha. Wakati wanafunzi wanasoma kwa sauti wanapaswa pia kufuata vitendo ambavyo alama za uandishi zinawakilisha. Mara wanafunzi wawili wakishamaliza zoezi hili, elekeza wanafunzi wengine zaidi waendelee na zoezi.

11Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

IGIZO (DAKIKA 20)

Sasa utafanya mazoezi ya mchezo wa alama za uandishi ambazo umezisoma kwenye Dhana Kuu. Unaweza kucheza mchezo huu darasani, nje au kwenye eneo la wazi.

• Mtu mmoja ataigiza kama ‘mwalimu’ mbele ya darasa wakati walimu waliobakia wataigiza kama ‘wanafunzi’ na lazima wasimame nyuma ya darasa (unaweza kuwa na washiriki zaidi ya wawili kwa wakati mmoja).

• Wanafunzi watembee polepole kutoka nyuma ya darasa kwenda mbele, na wakati wakitembea, mwalimu aliyeko mbele atashikilia kadi tofauti za alama za uandishi.

• Kwa kila kadi ya alama za uandishi, wanafunzi watapaswa kuigiza vitendo ambavyo alama hizo zinawakilisha. Kwa mfano:

1. Mkato ( , ) inaonesha kwamba wanafunzi wanapaswa kutulia kidogo na kisha waendelee kutembea2. Kituo kikuu (.) inaonesha kuwa wanafunzi lazima waache kutembea hadi uwaambie waanze tena.3. Alama ya mshangao ( ! ) inaonesha kuwa wanafunzi lazima waache kutembea na kuruka juu na

chini kwa shauku4. Alama ya kuuliza( ? ) inaonesha kuwa wanafunzi lazima waache kutembea na kisha wanyooshe

mikono yao hewani wakijaribu kugusa dari 5. Alama za kunukuu ( “ “) inaonesha kuwa wanafunzi lazima wapunge mikono yao hewani wakati

wakitembea

• Kama una darasa pana, mwalimu anaweza kushikilia baadhi ya kadi tofauti wakati wanafunzi wanatembea kutoka nyuma ya darasa kuja mbele. Elekeza wanafunzi waendelee kutembea baada ya kuwa wamesimama

• Mwalimu alieleze darasa kwamba mchezo huu ni sawa na wakati mtu anasoma. Wakati wanafunzi wanatembea, wanapaswa kufuata vitendo ambavyo alama za uandishi zinawakilisha. Wakati wanafunzi wanasoma kwa sauti, wanapaswa pia kufuata vitendo ambayo alama za uandishi zinawakilisha.

• Soma kipande cha matini chenye alama mbalimbali za uandishi

12 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

FIKIRI - WAWILI WAWILI - SHIRIKISHANA (DAKIKA 10) Baada ya kumaliza mchezo, jadili maswali yafuatayo hapa chini pamoja na mwenzako.

1. Ni namna gani alama za uandishi zinahusiana na ufahamu wa kusoma kwa ufasaha ?2. Namna gani mchezo huu unachangia kuboresha ufundishaji wako wa alama za uandishi darasani kwako?

13Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

KUAANDAA KIPINDI CHA “KUSOMA NA KUANDIKA” (DAKIKA 15)

Ili kukuza uwezo wa wanafunzi kusoma, ni muhimu sana kwamba aweze kufanya mazoezi juu ya mbinu mpya za kusoma na kuandika alizosoma kutoka kwenye Mafunzo ya Walimu Kazini.

Kurasa zifuatazo zinajumuisha masomo ya jumla yanayoelekeza shughuli ambazo unaweza kujaribu wakati wa kipindi chako cha kusoma na kuandika (au unaweza pia kujaribu wakati wa kipindi chako cha kawaida cha Kiswahili). Pamoja na mwenzako:

1. Soma kwenye mpango wa masomo.2. Jaza nafasi zilizo wazi mahali panapohitaji hivyo.3. Jaribu masomo wakati wa kipindi cha kusoma na kuandika.

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

MAANDALIZI

1. Kabla ya siku ya somo, chagua matini rahisi ya kusoma pamoja na wanafunzi wako. Hii inaweza kuwa aya fupi au shairi ambalo linajumuisha msamiati unaofahamika na maneno yanayosomeka.

2. Andika matini uliyoichagua ubaoni ikiwa na ukubwa wa kutosha kumfanya kila mwanafunzi aone. Mfano:

Sokoni Jana, nilikwenda sokoni na mama na baba yangu.Niliona kuku, mboga na matunda.

MUHTASARI 1. Tambulisha matini kwa wanafunzi. Soma kichwa cha habari na eleza kwa kifupi kinahusu nini. Kwa mfano, “Hadithi hii inaitwa, ‘Sokoni’. Vitu gani unaviona sokoni?”

2. Anza na ‘Ninafanya’: Waambie wanafunzi kwamba utaanza kwa kuwasomea kwa sauti. Soma hadithi kwa sauti na kwa ufasaha, onesha kwa kidole au kionesheo kwenye kila neno.

3. Hakikisha unasoma kwa kasi ambayo inahitajika kwa wanafunzi, soma maneno kwa usahihi, na soma kwa hisia kadri uwezavyo. Kwa hakika onesha wanafunzi wako kusoma kwa ufasaha kunamaanisha nini!

KUTAMBULI-SHA MAARIFA

MAPYA

1. Endelea na ‘Tunafanya’: Waambie wanafunzi kwamba ni wakati wao kuungana na wewe katika kusoma. Wanapaswa kufanya kila wawezalo kusoma kwa kasi ileile, usahihi na kwa hisia kama ulivyowaonehsa katika usomaji wa awali. Onesha kila neno kwa kidole au kionesheo.

MWONGOZO WA SOMO LA KWANZA: Kusoma kwa sauti pamojaHATUA ZA KUFUNDISHA

14 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

KUIMARISHA/KUKUZA MAARIFA

1. Malizia na Mnafanya’: Waambie wanafunzi kwamba watasoma kwa pamoja bila wewe. Unaweza kuonesha kidole kwenye neno au karibisha mwanafunzi kuonesha maneno wakati darasa likiyasoma.

KUFANYA MAZOEZI

1. Mwisho, waambie wanafunzi kwamba wanaweza kusoma wawiliwawili. Watabadilishana kusoma katika mistari ya matini. Wanafunzi watageuka kwa wenzao. Mwanafunzi mmoja anasoma mstari wa kwanza, kisha mwanafunzi mwingine anasoma mstari wa pili, na wanaendelea hadi wanamaliza matini. Wanafunzi wanapaswa kusomeana wao kwa wao tu, kwa hiyo wakumbushe kuongea kwa sauti za chini (lakini bado waoneshe hisia ).

KUPIMA MAARIFA

1. Mwisho wa somo, unaweza kufanya tathmini ya haraka kwa kuoneshea kidole kwenye sentensi moja tu kwenye matini na kuwaelekeza wanaojitolea wasome kwa sauti

2. Huhitaji kuonesha kidole kwenye sentesi kwa mfuatano. Wanafunzi wanapaswa kuwa na uwezo wa kusoma sentensi moja kwa kasi, usahihi na kwa hisia

3. Kama wanafunzi wanasoma polepole sana au bila usahihi, unajua kuwa wanahitaji kusaidiwa kuhusiana na kusoma maneno mengi ya kawaida.

4. Kama wanafunzi hawasomi kwa kujieleza, endelea kuwaonesha namna wanafunzi wanavyopaswa kujieleza wao wenyewe wakati wakiona alama fulani ya uandishi.

Tathmini:

Maoni:

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

MAANDALIZI

1. Kabla ya siku ya somo, hakikisha ukuta wako wa maneno umeboreshwa na maneno ya msamiati na maneno ya kawaida ambayo wanafunzi wamejifunza hivi karibuni. Kwa mfano:

MWONGOZO WA SOMO LA PILI: Kuunda sentensiHATUA ZA KUFUNDISHA

UKUTA WA MANENO

Maneno ya kawaida Maneno ya msamiatikwana

mamababakula

somalala

shulekakadadapika

semaonaita

JikoViatu

MwalimuKitabumeza

kimbiaelewa

15Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

MUHTASARI

2. Waambie wanafunzi kwamba watakuwa wanatumia maneno wanayoona kwenye ukuta wa maneno kuandika sentensi katika kundi

3. Gawa darasa katika makundi 2 – 5 ya wanafunzi (kulingana na ukubwa wa darasa lako). Kama unaweza, jaribu kuwaweka wanafunzi wanaojifunza polepole pamoja na wale wanaojifunza haraka.

4. Waambie wanafunzi watumie kipande cha karatasi kutoka kwenye madaftari yao. (Kama wanafunzi wako hawajaanza kujua kuandika, unaweza kufanya zoezi hili kwa kutamka)

KUTAMBULISHA MAARIFA MAPYA

5. Lieleze kundi kufanya kazi pamoja kufikiri sentensi mpya ambayo inatumia walau maneno matatu au zaidi kutoka kwenye ukuta

6. Lieleze kundi kwamba linapaswa kuandika sentensi kwenye kipande cha karatasi na pia lijumuishe alama za uandishi.

7. Waeleze wanafunzi kwamba unaweza kuwasaidia kwenye sentensi zao. Zunguka katika makundi yote wakati yanaendelea kuandika

8. Waambie wanafunzi kwamba wakati watakapomaliza, watapaswa kushikilia karatasi hewani.

KUIMARISHA/KUKUZA MAARIFA

9. Makundi yote yakishamaliza kuandika, alika kundi lisome sentensi zao kwa pamoja kwa ajili ya darasa zima. Wasisitize kwamba watapaswa kusoma sentensi zao kwa hisia

10. Baaada ya makundi yote kumaliza, elekeza makundi yabadilishane karatasi zao pamoja na makundi mengine. Makundi sasa yatapaswa kugeuka na kusoma sentensi zao mpya kwa sauti na kwa kujieleza kwa ajili ya darasa zima.

KUFANYA MAZOEZI

11. Rudia zoezi lakini waambie wanafunzi kwamba watapaswa kuandika sentensi mpya ambazo hazitajwa

12. Waambie kwamba wanaweza kuongeza maneno mapya kama inawezekana na kwamba unaweza kusaidia kuyaandika.

13. Wanafunzi wakikuomba uwasaidie kuandika neno jipya, jaribu kuwafanya walifiche neno: kwanza bainisha kila sauti ya herufi kwenye neno, na andika herufi ambayo inaendana na kila sauti.

14. Wanafunzi wote wakishamaliza, waambie wasome sentensi zao mpya (kwa hisia ) kwa darasa zima.

KUPIMA MAARIFA

15. Ndani ya somo hili, unaweza kuzunguka darasani kuangalia wanafunzi gani ambao wanapata shida na msamiati na kusoma kwa hisia .

16. Kuwa huru kuwabadilisha wanafunzi kwenye makundi ili wanafunzi wanaojifunza popote wapate fursa ya kukaa na wale wanaojifunza haraka.

17. Weka kumbukumbu ya msamiati ambao unatoka kwenye ukuta neno ambao wanafunzi hawakuutumia katika sentensi zao. Hii inaweza kuonesha kwamba wanafunzi wanakumbuka au wanaelewa maana ya neno. Kwa hiyo, fikiri kuhusu kurudia kuwafundisha wanafunzi hao.

Tathmini:

Maoni:

16 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUTENGENEZA VITABU VIKUBWA(DAKIKA 45)

Sasa, utakamilisha kitabu kikubwa ambacho ulipanga kwenye kipindi chetu cha mwisho. Kumbuka: vitabu vikubwa ni vitabu ambavyo vina picha kubwa na maneno makubwa. Ukubwa wa picha na maandishi vinawasaidia wanafunzi kuweka mkazo na kufuatilia hadithi wakati wanajifunza kusikiliza. Vitabu vikubwa vina faida kutumia katika darasa kubwa ili wanafunzi waone na kushiriki katika kutambua maandishi na maelezo wakati wanasoma. Kukamilisha kitabu kikubwa, utahitaji vifaa vifuatavyo:

VIFAA VYA KADI YA PICHA

√ Karatasi 3 – 5 za A2√ Penseli√ Karatasi ya bodi ya hadithi ambayo ulikamilisha katika kipindi kilichopita√ Viweka alama na rangi√ Mkasi√ Kamba

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHA

Katika kipindi hiki, kuwa huru kuwa na walimu wawili wakifanya kazi pamoja kuandaa kitabu kimoja.Mnaweza kufanya kazi pamoja kutengeneza kitabu kingine katika muda mwingine.

HATUA YA 1: Kunja kurasa za bango karatasi na andika namba za kurasa. Kila ukurasa wa bango karatasi ukunjwe kwa nusu. Na kila nusu itakuwa ukurasa mmoja kwa kitabu hiki. Kwa hiyo, kama ulipanga kuwa na kurasa 6 katika kitabu chako, kunja kurasa 3 za bango karatasi. Andika namba za kurasa (anza kutoka ukurasa wa pili) chini ya kila ukurasa.

HATUA YA 2: Anza kutengeneza Kitabu Kikubwa kwa kutengeneza “Ukurasa wa Kichwa cha habari” Kurasa za vichwa vya habari hujumuisha kichwa cha habari chenyewe, jina la mwandishi, na maelezo yanayoibua mandhari na mawazo muhimu ya hadithi za Kitabu Kikubwa. Hupaswi kuandika namba ya ukurasa kwenye ukurasa wa kichwa cha habari.

HATUA YA 3: Nenda kwenye karatasi yako na andika maandishi ya kitabu chako kwenye kurasa za kitabu Tumia karatasi uliyoiandaa kuandika hadithi yako kwenye kurasa za kitabu chako. Sentensi hizi ziandikwe vizuri na kwa herufi zilizochapishwa (siyo kuvirigishwa) chini ya ukurasa.

17Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHA

HATUA YA 4: Eleza kwa mifano kwenye kitabu Katika kila ukurasa, chora picha ambayo inawakilisha maandishi uliyoandika. Kama kuna maneno ya msamiati wowote katika hadithi yako ambayo yanaweza kuoneshwa ana kwa ana, hakikisha unayajumuisha katika mifano yako. Maelezo haya ya mfano hayapaswi kuwa na taarifa nyingi au yaliyosanifiwa, lakini yanapaswa kuhusiana na maneno yaliyoko kwenye ukurasa. Kama hauna uwezo wa kumaliza maelezo ya mifano yako yote wakati wa kipindi hiki, usiwe na wasiwasi. Utakuwa na muda mwishoni mwa moduli inayofuata ya 14 kumalizia Kitabu Kikubwa.

HATUA YA 5: Bana Kitabu KikubwaTumia mkasi au skurubu kutoboa matundu mawili kwa kufuata mikunjo ya bango karatasi. Ingiza kamba kupitia katika matundu na funga mwishoni ili ukurasa ukae mahali pake.

18 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHA

HATUA YA 6 - (Kama muda unaruhusu): Soma kitabu kikubwa pamoja na washirika Kumbuka kutumia mbinu za kusoma zilizojadiliwa kwenye moduli ya 5:

• Shikiliakitabukikubwakuliakwakoaukushotoiliwanafunziwotewaone• Ulizamaswalikuhusukichwachahabarichakitabukikubwakablayakusoma

(wanafunzi wanafikiria hadithi inahusu nini)• Jadilichapishokwenyeukurasawajuu(kichwachahabari,mtunzi,muwekavielelezo)• Onesheakidolekwenyemanenowakatiunasoma• Somakwakujielezakwashauku• Ulizaswali1kwakilaukurasawakatiunasoma• Ulizamaswalibaadayakusoma

UFUATILIAJIBaada ya kumaliza moduli hii, Mratibu Elimu wa Kata, Ofisa Elimu wa Wilaya na Mkaguzi wa wilaya watafuatilia kuona namna unavyotumia mbinu za moduli hii katika darasa lako. Wakati wa ufuatiliaji huu, ni muhimu uwe na uwezo wa kuonesha mambo yafuatayo:

a) Kueleza mbinu za kukuza kasi, usahihi na hisia .b) Kueleza mbinu ya KUFUNDISHA alama za uandishi na kufafanua namna

zinavyohusiana na kusoma kwa hisia .c) Kuonesha Kitabu Kikubwa ulichotengeneza. d) Kuonesha namna ulivyotumia mpango wa masomo wa moduli hii kwenye

darasa lako.

19Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MWISHO

MWISHO (DAKIKA 10)Binafsi jaza fomu ifuatayo kuweka rekodi ya tathmini ya moduli ya leo. Baada ya kukamilisha, chomoa ukurasa huu na umpe Mratibu wako. Tafadhali uwe mkweli kwa vile mrejesho wako utasaidia kuboresha Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule hapo baadaye.

JEDWALI LA KUTATHMINI Alama 0:

Sikubaliani kabisa na usemi huu

Alama 1: Kwa kiasi Sikubaliani

na usemi huu

Alama 2:Nakubaliana kwa kiasi na usemi huu

Alama 3: Nakubaliana Kabisa

na usemi huu

FOMU YA TATHMINI

Shule: ______________________ Wilaya: ___________________ Mkoa:_____________________

Tathmini ya Moduli: ________ Mada ya Moduli: ______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki: ________ Mwalimu Mkuu alishiriki: Ndiyo/Hapana

Mratibu alikuwepo kuwezesha: Ndiyo/Hapana

Soma semi zifuatazo kisha weka alama ya vema katika kisanduku husika kuonesha jibu lako:

0 1 2 3

1. Dhana kuu ya moduli ya leo ilikuwa inaeleweka.

2. Moduli hii ina mikakati mingi mizuri na yenye manufaa ambayo nitaitumia darasani kwangu.

3. Muda uliotumika kukamilisha moduli hii unafaa. Sikuhisi kwamba ni muda mrefu sana.

4. Moduli hii iliibua mjadala wa kufurahisha na tafakuri ya hali ya juu sana.

5. Violezo vya kipindi cha kusoma na kuandika vilisaidia sana. Natarajia vitakuwa rahisi kuvitumia ndani ya darasa langu.

6. Zana tulizotengeneza leo zitakuwa za manufaa sana (kama inahusika).

7. Mratibu amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia.

8. Mratibu anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu.

9. Mratibu anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika.

10. Mratibu anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini Mafunzo ya Walimu Kazini ni muhimu kwetu.

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule