17
CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA UNITED KINGDOM Email [email protected] Tel+44 78 33571100. Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza. MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nchini Uingereza Ndugu Kangoma H Kapinga (KK). Kamati kuu ya CCM iliridhia kuanzishwa kwa matawi nje ya Tanzania kule ambako kuna wanachama na wapenzi wa kutosha wa CCM takribani miaka 9 iliyopita. Nchi ya kwanza kufungua tawi ilikuwa ni UK (wakati huo CCM London) na kuanzia hapo CCM UK/01/2015

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Embed Size (px)

DESCRIPTION

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Citation preview

Page 1: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nchini Uingereza Ndugu Kangoma H Kapinga (KK).

Kamati kuu ya CCM iliridhia kuanzishwa kwa matawi nje ya Tanzania kule ambako kuna wanachama na wapenzi wa kutosha wa CCM takribani miaka 9 iliyopita. Nchi ya kwanza kufungua tawi ilikuwa ni UK (wakati huo CCM London) na kuanzia hapo matawi mengine yalifunguliwa sehemu zingine duniani ambako kulikuwa na wanachama au wapenzi wa CCM.Nini hasa ilikuwa vision/lengo la kamati kuu kuruhusu ufunguzi wa matawi hayo?Je lengo limetimia? Nani anatakiwa kupima viwango hivyo? Kamati kuu yenyewe au wapenzi wanaccm katika matawi hayo?Mimi kama kiongozi wa sasa wa CCM UK nimetafakari kwa kina hali halisi ya mwenendo wa matawi haya (diaspora) na kuona kuwa nina jukumu la kuandika chochote

CCM UK/01/2015

Page 2: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

ili kisomwe na wadau wa CCM diaspora na pia napenda kufungua hoja hii makusudi ili wengi wetu tuweze kuendeleza mjadala huu kwa manufaa ya chama chetu na matawi ya diaspora ili kupata namna bora ya kuendeleza shughuli za chama kwenye diaspora na hivyo kupata majibu ya maswali niliyouliza hapo mwanzoni.

Ni dhahri chama chochote cha siasa hupendwa na wananchi kutokana na uwezo wa taasisi hiyo wa kubuni na kujitahidi kutekeleza agenda ambazo zinawahusu watu wake. Chama ambacho sera na mikakati yake haikidhi matarajio ya watu wake, idadi ya wanachama wake hupungua siku hadi siku. Na matarajio hayo ya wanachama hutofautiana kutokana na tabaka lao; kwa mfano wakulima wadogo wana mahitaji tofauti na wakulima wakubwa hali kadhalika kada zingine za kwenye jamii hiyo hupokea sera zinazowapendeza kwenye tabaka husika.

Ni nini mahitaji ya wanachama na wapenzi wa CCM kwenye diaspora??

Wana-diaspora wengi wapo huku kwa sababu za kijamii na kiuchumi, hivyo kwa ccm kuweza kuendelea kuwa na wanachama na wapenzi wake kwenye diaspora ni lazima chama kujipanga vizuri kwenye agenda hizo ili kiweze kujijenga kwenye tabaka hilo muhimu. Na hakika waTanzania wengi kwenye diaspora wamefanikiwa kuondokana na dhiki mbalimbali kwani wana vipato vya kuridhisha na kuweza kumudu mahitaji yao na ya familia zao hata kule nyumbani. Na wengi wanategemewa sana na familia zao huko Tanzania na wapo waliovuka viwango vya familia na hata kuhudumia jamii pana Zaidi kule nyumbani; wapo waliosaidia kwenye shule, miradi ya maji na huduma mbalimbali za jamii husika. Kwa kifupi mahitaji ya wana-diaspora ni Zaidi ya chai na mkate!Ili kuelezea hoja yangu vizuri ni bora nikaichambua kidogo jamii yenyewe ya diaspora (Ulaya na Amerika) na kwa uelewa wangu ina makundi kama matatu;

1. Kundi la kwanza lilikuja diaspora kwa makusudi ya kujikomboa kiuchumi moja kwa moja na hao wapo kwenye makundi madogo mengi tu ikiwa ni pamoja na kutumia njia za ukimbizi na aina zinguine za uhamiaji. walijiingiza kwenye kazi yoyote waliyoikuta ili mradi mahitaji yao ya kijamii na kiuchumi yapatikane na waliweza ku-leta wategemezi wao kama watoto na hata wadogo zao.

2. Kundi la pili lilikuja kusoma na wengi wao walifanikiwa kumaliza shule zao lakini hawakurudi tena Tanzania bali walijiunga na maisha ya diaspora. Na kwa kweli kundi hili ndilo kubwa na iliwachukua watu hao muda mrefu Zaidi kujihalalisha rasmi kwenye mfumo wa maisha ya nchi husika (citizenship).Na wengi wana knowledge ya kutosha. Makundi hayo mawili pamoja na kuwa na elimu pia yamefundishwa stadi mbalimbali za kazi kwenye mazingira ya uzalishaji wa kisasa (best practice) hivyo wengi wao ni mabingwa wa kutumia zana mbalimbali za kisasa za uzalishaji na katika sekta za huduma huku kwenye diaspora.

CCM UK/01/2015

Page 3: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

3. Kundi la tatu ni la vijana wanaotokana na makundi mawili ya mwanzo; yaani watoto na hata wategemezi wao. Na hilo ndilo kundi linalochipukia kwa sasa nami sitasita kuliita 2nd generation ya diaspora ya Tanzania. Wengi waliopo kwenye kundi hilo hawana matatizo ya msingi kama ya makundi ya mwanzo kwani wao walinufaika moja kwa moja na waliowatangulia (wazazi au wasimamizi wao) hao wamesoma bila vikwazo kwa aliyehitaji elimu na wengi wao wapo kwenye vyuo vya elimu kwenye vi-wango mbalimbali. Tatizo kubwa la tabaka hili ni kutokuwa na habari za kutosha kuhusu nchi yao ya asili (Tanzania) na wengi wana mapenzi na nchi yao (hiyo) ya asili na wangependa kwenda kuitumikia kwenye sekta mbalimbali wakati utakaporuhusu.

HALI YA CHAMA KATIKA MASHINA YETU: Kuna aina nyingi za wanachama tuliowapata kwenye mashina ya diaspora; sehemu kubwa ya wanachama hao wanatokana na :

Kundi (a). Wapenzi na wanachama wa ccm waliotoka huko Tanzania ambao walihamishia uanachama wao mara moja kwenye mashina yetu ya diaspora, naKundi (b). Watanzania waliohamasika na uzalendo wa nchi yao ambao walidhani kujiunga na ccm kwenye diaspora ni njia mojawapo ya kuimarisha mshikamano miongoni mwetu huku kwenye diaspora.

Sasa nini kifanyike kuongeza wanachama kwenye diaspora ndilo suala ambalo sisi viongozi tunatakiwa kuliangalia kwa makini. Tujiulize pia tufanye nini ili kuwafikia vijana niliowataja kwenye kundi la tatu hapo juu kama tunataka kuongeza idadi ya wanachama .Na je kamati kuu/ Halmashauri kuu yenyewe ya ccm kwenye dia-spora yetu inao uwezo wa kusukuma dhana yenyewe ya ccm matawi ya nje? Je tuna uelewa wa kutosha kuhusu sera za chama chetu?

Kwa kweli sisi viongozi huku kwenye diaspora tunajukumu kubwa la kueneza na kuzitetea sera za chama cha mapinduzi kijamii, kisiasa na kiuchumi. Mashina ya di-aspora lazima yawe na viongozi wanaoelewa na wako tayari kujifunza kila siku ili wawe ’point of contact’.

KIJAMIINi lazima viongozi wa ccm kwenye diaspora wawe ni watu wanaounganisha watanzania katika miji yao wakati wa shida na raha ili kuwafanya watanzania waone kuwa ni sehemu muhimu ya jamii yao. Wawe ’reliable and trustworthy’ na kuwafanya wawe ni kimbilio la Wanachama na watanzania kwenye mambo muhimu kama habari za misiba na hata graduation za watoto wetu na pia ku-

CCM UK/01/2015

Page 4: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

saidia kutambulisha vipaji mbalimbali vya watoto wetu ‘talents’ kwenye jamii husika na ndipo tutaweza kuwavuta wazazi na watoto wenyewe kuja upande wetu na hivyo kuongeza umaarufu wa chama katika ngazi hizo.

KISIASA:Viongozi wa mashina lazima wawe na weledi na ufahamu wa kutosha kuhusu maendeleo ya nchi yetu yanayosimamiwa na chama cha mapinduzi. Panapo-tokea mkanganyiko wa habari kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi kwenye jamii ccm diaspora lazima ishike hatamu ya kuelewesha jamii na kuondoa hisia potofu kuwa ccm ni chama cha wezi kama wapinzani wetu wanavyotaka kupo-tosha.

Ninayo mifano miwili ya vijana ambao hapo siku za nyuma walikuwa ni wagumu kujiunga na jamii zetu kama ccm,mmoja ni kijana nilimfahamu kwenye mji wa Reading ambaye alikuwa anamwaga maneno machafu kuhusu uongozi wa nchi yetu pamoja na chama chetu chama mapinduzi kuwa wa hovyo na hawafanyi chochote kwenye maendeleo ya nchi yetu, na wa pili kijana ambaye nimeishi naye kwenye mji wa Southampton kwa muda mrefu sasa na ambaye alikuwa anakiponda chama chetu pamoja na uongozi wake huko nyumbani na hivyo ku-tuona hata sisi ambao tunaongoza chama kwenye diaspora hatufai! Lakini siri ni kwamba vijana hao wote wawili hawakuwahi kurudi nyumbani kwa miaka mingi kutokana na matatizo mbalimbali, Vijana hao wote wamefanikiwa kwenda ny-umbani miezi michache iliyopita na wamerudi wakiwa ni watu tofauti kabisa!!! Wote wanaisifu nchi yetu na wanakubali kuwa ccm imeleta maendeleo mak-ubwa na raisi wetu amefanya kazi nzuri sana na wameahidi kurejea nyumbani kuangalia fursa mbalimbali.

Muono wa vijana hao wawili pia wanao vijana wengi pamoja na watanzania wa kwenye diaspora ambao hawajabahatika kufika nyumbani miaka mingi. Kwa maoni yangu ccm diaspora lazima iwe na habari za kutosha kuhusu maendeeo ya sekta mbalimbali, kuwe na uelewa wa kutosha kuhusu ilani ya uchaguzi wa chama chetu na mambo yote yanayotekelezwa ili kuweza kutoa majibu kwa wale wenzetu ambao hawapati bahati ya kurudi nyumbani kwa sababu mbalimbali.

Tutumie mitandao ya kijamii na uwepo wetu kwenye miji mbalimbali kukusanya habari sahihi kuhusu maendeleo ya Tanzania kisiasa na kijamii wakati huohuo

CCM UK/01/2015

Page 5: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

lazima tuwe wakali na kukosoa viongozi mbalimbali kule nyumbani na kwenye taasisi za serikali wanakuwa chanzo cha ccm kupakwa matope. Tufanye hivi kwa kufuata taratibu zetu za kichama na hata ikibidi kutumia mitandao ya kijamii ku-laani viongozi wasio waaminifu wanaokipaka chama matope kwa matendo yao.

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu kule nyumbani. CCM diaspora isinyamaze huku na kuacha viongozi waovu waingie ikulu! Tusaidie kutoa elimu kwa viongozi na wajumbe mbalimbali wa mkutano mkuu kupitia channels mbalimbali ikiwa ni pamoja na influence kwenye mikoa na wilaya mbalimbali ili apatikane kiongozi mwenye maadili na uwezo wa kusukuma gurudumu la nchi yetu ipasavyo na pia kulinda heshima ya nchi yetu iliyojengwa kwa miaka mingi. Pia tufanye hivyo kwa kufuata utaratibu (ethical) ili kuto kuwapaka watu ma-tope na/au kutumiwa na makundi yanayopinzana. Tuwe na semina na mikutano ya mara kwa mara kuweza kupeana habari kuhusu maendeleo ya nchi yetu yanayosimamiwa na ccm na pia tuwe mabalozi wa chama katika diaspora husika.

KIUCHUMI:Watanzania kwenye diaspora kama nilivyoandika hapo juu wametumia muda mwingi sana uliopita kupigania uhalali wa kuishi kwenye nchi husika (citizenship),Sasa ni lazima wahamasishwe ili waweze kuingia awamu ya pili ya maisha halisi ya kwenye diaspora zao ambayo ni ‘economic engagement’. Vikao vyetu vitumike kupeana habari mbalimbali za kifursa, ili baadhi yao waingie kwenye uchumi mkubwa kwa kuingia kwenye ujasiriamali.

Hii ndio kada inayokosekana miongoni mwa wa-Tanzania wa kwenye diaspora. Yaani kuweza kuwafanya wakatumia uwepo wao kwenye masoko makubwa kama ya hapa UK ili kuwa kiungo kwa makampuni au huduma mbalimbali zinahusika na makampuni hayo ulimwenguni pia hata nyumbani! Tuwasaidie kuweza kujenga mtandao na makampuni ya kule nyumbani na kuweza kujua demand zao za kibi-ashara au ku-extend service mbalimbali kwa faida ya pande zote mbili (win-win); yaani faida iweze pia kuwafikia wao wenyewe na vizazi vyao hapa kwenye dia-spora na nyingine iende kwenye taasisi husika.

Hivyo viongozi wa mashina ya ccm lazima wawe mbele katika kuwahamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kushiriki forums mbalimbali zinazojitokeza sio lazima ziwe za kitanzania pekee!! Pia tuandae forum na makampuni ambayo

CCM UK/01/2015

Page 6: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

yanaweza ku-hire skills za watanzania na kulipwa vizuri ili best practice zetu zi-weze ku-flow kwenda kwenye taasisi hizo nyumbani kwa faida ya pande zote mbili. Kwa ujumla tuwe sehemu muhimu ya uanzishwaji wa dhana ya diplomasia ya uchumi kwa nchi yetu.

CHANGAMOTO: Na hakika waTanzania kwenye diaspora wana ujuzi wa taaluma mbalimbali na wamepata mafunzo yanayowafanya waweze kutoa huduma katika masoko mak-ubwa katika nchi husika. Miongoni mwao ni PAUL;-( mtanzania) nilimkuta nikiwa nasafiri na train ya Crosscountry kutoka Birmingham nikielekea Manchester Pic-cadilly ndipo nilipomsikia akijitambulisha kuwa yeye ni service manager wa route hiyo!

PAUL amepewa dhamana ya kuhakikisha kuwa wasafiri wote wanaotumia train hiyo wanapata huduma bora inayolingana na walicholipia (Value for money), Na watanzania wa aina ya PAUL wapo wengi tu huku diaspora wenye majukumu kama hayo na hata Zaidi ya hayo na wamepata mafunzo ya fani mbalimbali yenye uwezo wa kutoa huduma katika soko kubwa kama la hapa UK.

Paul sio mwajiriwa wa kampuni kubwa ya Crosscoutry trains bali ni kampuni ndogo tu lakini yenye uwezo wa kutoa huduma kwa wateja wa kampuni kubwa kama ya Crosscoutry trains. Na kilichoisaidia kampuni hiyo ndogo kupata tenda hiyo sio kujuana au kupigiwa pande na mzito wa serikali ya UK, Bali ni mazingira

sawa ya kifursa au kwa kiingereza Levelled Playing Field (LPF). Ambapo wenye sifa na uwezo wa kutekeleza jukumu Fulani ndio wanaopewa nafasi ya kuchukua hiyo fursa. Akina PAUL na Watanzania wengine ndio wanaoogopa kurudi nyum-bani kwa kuogopa kuwa hawatakuwa na nafasi sawa za kifursa kwenye jamii pamoja na kuwa na ujuzi na uwezo wa kutoa huduma za kiwango cha juu kwa sab-abu wanaamini nyumbani hakuna LPF.

Hivi karibuni tumeshudia shirika la reli likiingiza mabehewa mapya ya kutoa hu-duma za uchukuzi kwa nchi yetu, Ni dhahiri watu wa kada kama za bwana Paul wanatakiwa wapewe mrahaba wa kutoa huduma kwenye train hizo ili kuleta mapinduzi ya huduma kwenye taasisi hizo. Wengi tunajua aina ya huduma zinazopatikana kwenye taasisi kama za TRC hivyo hata kama mabehewa yatak-uwa mapya hatutarajii huduma bora kutoka kwenye taasisi hiyo kama sio kuleta

CCM UK/01/2015

Page 7: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

wageni toka India au kwingineko,hivyo sisi viongozi wa diaspora pia tunatakiwa kupigania watu wetu ili kuhakikisha kila inapobidi wapewe fursa hizo na hii ndiyo LPF ninayoizungumzia.

HALI HALISI YA TANZANIA:Mimi ni mmoja wa Watanzania wanaosafiri mara kwa mara kuja nyumbani na hakika sa-fari zangu hazikomi Dar peke yake huwa mara zote naenda hadi huko Mbinga kijijini kwangu kwa asili. Kwa hakika ninalo la kuwaambia wenzangu wa diaspora ni nini kin-aendelea kwenye uchumi wa nchi yetu. Kwa kifupi nchi yetu bado ni salama na nzuri kwa maana ya hali ya hewa na usalama wa raia.

Nina hakika hata mali asili nyingi bado zingalipo tofauti na wengi wetu tunavyodhani. Ukitoka songea mjini kuelekea mbinga katikati yake utakutana na wawekezaji wakubwa wa kilimo cha kisasa na hata vijana wanaochimba madini kwa kutumia zana duni sana lakini wanapata wanachofanikiwa kupata. Nadhani hata huko mererani na kwingineko hali ni hiyo. Bado mito na maziwa yetu makuu hayajatumiwa ipasavyo kwa uvuvi na kilimo cha umwagiliaji. Bado milima na mabonde yetu hayajatumiwa vya kutosha kuzal-isha bidhaa nyingi na kuyafikia masoko makubwa kama ya huku diaspora, na vijiji vyetu bado vinakaliwa na wakulima na wafugaji wadogo.

Hivyo mtaona kuwa moja ya tatizo kubwa la nchi yetu ni uzalishaji mdogo unaotokana na zana duni na maarifa kidogo (primitive production) lakini kilicho wazi pia ni ukosefu wa masoko ya uhakika ya bidhaa hizo! Ni juzi tu nimesoma kuwa huko New York wauzaji wakubwa wa madini yetu ya Tanzanite ni India kiasi cha USD 600, wakifuatiwa na Kenya kiasi cha 300USd na sisi wenye madini hayo tunaambulia ‘market share’ as-ilimia kidogo sana. Wafanyabiashara wa India hawapelekwi huko Mererani na serikali yao na wala wenzetu wa kenya hawatumwi na chama tawala cha nchi yao bali ni ujasiria mali tu, wanalijua soko na wanatafuta bidhaa iliko basi.!! Watanzania wen-zangu tunashindwa wapi? Ccm diaspora lazima ianze kuongoza mijadala ya kuzitam-bua fursa hizo kwenye sekta ya madini. Kwa mfano ni kwenye sekta ya uchimbaji mdogo wa madini tuwahamasishe wanachama wetu waweze kutafiti zana mbalimbali zinazotumika kwenye utafutaji wa madini hayo na kwa vile sasa serikali imedhibiti utoaji holela wa madini kuja kwenye masoko ya nje upenyo ambao wageni walikuwa wanautumia kusafirishia madini yetu hivyo ‘Vacuum’ hiyo lazima izibwe na wanadiaspora kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaisaidia pia nchi yetu kukusanya kodi mbalimbali. Na sisi wenyewe kujihusisha rasmi na uuzaji wa mali hizo. ‘Mali za Tanzania ziuzwe na watanzania wenyewe’

CCM UK/01/2015

Page 8: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

Pia wanadiaspora wengi hatujui tena mikoa yetu ya asili kila mmoja anazungumzia Dar pekee! Mnyamwezi wa Tabora yupo diaspora hajishughulishi na kutafuta soko la asali kwa vile hana habari sahihi kuhusu uzalishaji wa asali kule kwao Tabora! Where is the missing link? Matawi ya nje ya ccm lazima yasaidie kupata majibu ya maswali haya, tusisubiri chama kingine kije kitoa majibu kwani tutakuwa tumechelewa na tusiruhusu watanzania mpaka waanze kutafuta sababu ya kumtafuta mtu wa chama kingine aje atoe majibu

CHANGAMOTO 2:Ni kweli nchi yetu ipo salama na inakwenda kwa kasi kimaendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Kuna miundombinu inayojengwa na serikali ya awamu ya nne ya chama cha mapinduzi na sasa nchi yetu inafikika kirahisi karibu se-hemu nyingi, ardhi yetu bado ni salama na inapatikana kwa bei nafuu huko mikoani japo ushindani wa kuipata unaongezeka siku hadi siku.

Hakika sisi wana- diaspora tuna nafasi ndogo sana iliyobaki ya kukutana na kupanga mi-kakati au kupeana taarifa sahihi za namna ya kujiingiza kwenye sekta rasmi za uzalishaji kule nyumbani na kwa wale ambao hawajahamasika kwenda kuwekeza huko nyumbani wanaweza kujiingiza kwenye masoko ya bidhaa mbalimbali toka Tanzania. Ni wakati sasa wa diaspora kuji-organize ili kama kuna taasisi za nyumbani zitakuja kutafuta namna ya kufanya kazi pamoja na wanadiaspora watukute tupo tayari. Tuzitambue fursa mbalimbali zilizoko kwenye sekta za uzalishaji kule nyumbani ili tuwe wa kwanza kwenda kuwekeza kila fursa inapoonekana badala ya kuwaachia wageni.

Moja ya sababu zinazotolewa na wengi ni kukosekana kwa mitaji! Katika sera zangu za matawi ya nje mara nyingi nimezungumzia suala la sisi wenyewe kwanza kuanza kuwekeza mitaji kwa njia ya umoja wa SACCOS na ndipo tutakuwa na jeuri ya kutafuta taasisi zinazoweza kutuunga mkono katika kuongeza mitaji hiyo. Wana-diaspora tujipange kiuchumi hakuna mtu atakaye kuja kutugawia mapesa ya uwekezaji na hata makampuni mengi hutoa mikopo kwa masharti ya mkopaji kuwa na kianzio, hivyo su-ala la SACCOS ni la muhimu sana na mimi kama kiongozi wa tawi la UK nimeshaanza maandalizi ya kuanzisha chombo hicho na ni wajibu wa viongozi wa mashina kuhamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kujiunga na kikundi hiki.

CCM UK/01/2015

Page 9: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

Pia biashara ya utalii kwa wale vijana wa kundi la tatu ambao wanahitaji taarifa sahihi kuhusu vivutio vyetu na aina ya vyakula vyetu ambavyo wanaweza wakasaidia kuvibore-sha na kufikia viwango vya kimataifa na kupendwa na watalii wanaokwenda nchini kwetu. Tunatakiwa kuingia masoko hayo bila kutumia taasisi za nyumbani kwani zina ukiritimba ambao utatukatisha tamaa kwani moja ya changamoto kubwa tulizonazo nchini kwetu ni ugumu wa taasisi hizo kuruhusu kuingiza watu wapya kwenye uchumi na kwa kweli kama tutasubiri LPF kutoka kwenye taasisi za serikali kule nyumbani ni dhahiri wanadiaspora tutaendelea kuwa watazamaji kwenye uchumi. Jitihada zitumike kuwa-hamasisha wanadiaspora kufanya maamuzi ya kujiunga na uzalishaji bila kuzibembeleza taasisi hizo zinazokumbatia ukiritimba.Tukutane nao sokoni!

Mfano ni majuzi nilikwenda pale Sunderland kushuhudia uzinduzi wa klabu hiyo kutu-mika kama tangazo la utalii kwa kushirikiana na bodi yetu ya utalii ya Tanzania (TTB) na baadae nilimtafuta Mkurugenzi mkuu wa TTB ili atusaidie kwenye diaspora tuwe na programme za vijana wale niliowataja kwenye namba 3 hapo juu ili waweze kufaidika na information za TTB kuhusu utalii wetu na vivutio vyake na baadae watumike kama mabalozi wa utalii wa Tanzania kwenye ground ya UK na hata baadhi yao kujiajiri kwenye sekta hiyo!

Programme iwe ni ku-extend nyenzo za TTB kama information fliers,na hata semina mbalimbali hukuhuku diaspora badala ya kutegemea wazungu pekee! Kwani vijana hao wana connection Zaidi na familia za hapa na wamesoma na wezao ambao ndio tabaka la watalii linalokuja, Jibu la yule mama(mkurugenzi) lilikuwa rahisi sana kwamba hawana mpango wa kuingiza ‘Ideas’ za mtu mwingine yeyote wao wenyewe TTB wanatosha kufanya kazi hiyo dunia nzima! Yule mama anashindwa kuelewa jinsi gani tunapaswa kujibu maswali makazini kwetu hapa diaspora pindi watu wana-pobaini kuwa tunatoka sehemu hiyo ya dunia, lakini kwa vile hatuna habari za kuto-sha kuhusu vivutio vyetu tunakwama kutoa majibu! haelewi kuwa tumechelewa sana kutangaza vivutio vyetu vya utalii na kuwa sasa tunahitaji kuongeza ‘pace’ ya kuit-angaza nchi yetu.

Ndugu zangu wa diaspora tukisubiri LPF tutakwama. Atitude ya kiongozi wa TTB pia wanayo viongozi wa taasisi nyingi kule nyumbani, Mindset zao sio kuongeza uzalishaji(production capacity) ili pato liongezeke litutoshe wote la hasha, bali wao ni wajuzi wa kugawa hicho kidogo kinachozalishwa tena kwa wachache na hawajali nani hakikumfikia!(Strict distribution of what is being produced) ndo maana hoja zao ni budget na inatokana na nani apewe na nani asipewe ‘’Haoni mantiki ya kupanua wigo

CCM UK/01/2015

Page 10: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

wa kutangaza utalii wa Tanzania ili watalii waende wengi na wapate huduma bora na hatimaye mapato yaongezeke na ndio tuweze ku-solve hilo tatizo la budget analolijua’’! Maadam wao na marafiki zao wanakula kutokana na hicho kidogo hawana haja ya kupigania kuongeza uzalishaji kitu ambacho ndo tatizo kubwa la nchi yetu; ”Uzalishaji mdogo’’.

Tuna viongozi wengi ambao ni mafundi wa kugawa hicho kidogo badala ya kuwa na vi-ongozi wanaoweza kusimamia kuongeza uzalishaji. Na ili kuongeza uzalishaji ni lazima makundi yote yanayoweza kusaidia kubuni na kusukuma uzalishaji mpya yaingizwe kwenye mikakati (system). Makundi kama diaspora lazima yasaidiwe ili yaweze kuingiza Skill/best practice zao kwenye sekta mbalimbali za uzalishaji na kusaidia kutengeneza kazi kwa vijana.Hivyo sisi kama viongozi wa ccm kwenye diaspora inatakiwa tukisaidie chama ku-organ-ize hili kundi ili liwe tayari kwa changamoto hizo. Maana ni rahisi kulalamikia ukiritimba wa serikali na taasisi zake lakini je tupo tayari?

Hivi karibuni niliona picha ya wazee wetu waliokuwa diaspora mwaka 1959 hapa Lon-don, walijikusanya na kuanzisha tawi la TANU hapa UK wakati huo! Majukumu ya wakati huo yalikuwa ni pamoja na kuhamasisha namna ya kuharakisha juhudi za kupata uhuru wa nchi yetu. Na kati yao kweli walikuja kuwa viongozi wa mwanzo wa Tanganyika huru, akiwemo mhesh. Mark Bomani na marehemu Oscar Kambona ninaowakumbuka kwenye ile picha yao ya London 1959. Kwa hiyo harakati za ukombozi zina historia na UK nami kama kiongozi wa ccm hapa UK nimeona ni bora tuanzishe harakati za ukombozi wa uchumi kwa wana diaspora hapahapa UK.

Tutumie fursa kadhaa ambazo serikali yetu imezitengeneza ili sasa tuanze kuyafikia masoko na pia kuanza kujenga tabaka la “knowledge economy” kwa nchi yetu maana nchi yetu inahitaji ’innovators’ kwenye sekta zote za uzalishaji Kuanzia kilimo,uvuvi,uchimbaji mdogo wa madini n.k ili kusaidia kupunguza tabaka la sasa la wazalishaji holela. Kwa manufaa yetu wenyewe na vizazi vyetu vya huku diaspora na kwa ndugu zetu kule nyumbani kwani tutakuwa chanzo cha ajira na kuhamisha hizo best practice kwenda kwenye vikundi vya uzalishaji kule nyumbani kwa njia ya partnership na vikundi vya huko. Kamwe tusiruhusu soko hilo lichukuliwe na wageni kwa kukosekana kwa watanzania wenye ‘knowledge and skill’. Zana zote za uzalishaji,uchukuzi na usafirishaji na hata viwanda vidogo zinapatikana huku tuliko, tujadili namna ya kupata mitaji sisi wenyewe ili tuondokane na urasimu wa

CCM UK/01/2015

Page 11: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

taasisi za serikali kule nyumbani! Kwa namna hiyo ndo tutakuwa tunakisaidia chama chetu cha mapinduzi kutekeleza kwa vitendo sera mbalimbali za uzalishaji wa kisasa.

Kuanzia sasa nataka mashina yetu yaanze kuweka agenda za kiuchumi na kijamii kwenye orodha ya mikutano wanayotarajia kufanya kwenye mashina hayo na hata kwenye vijiwe vyetu kwenye miji mbali mbali maongezi yaanze kubadilika nitajitahidi ku-organ-ize semina za viongozi ili tuweze kuongeza uelewa kwenye Nyanja hizo. Narudia tena technology zote zinazotumika kwenye uzalishaji duniani zinatoka kwenye nchi hizi tunazoishi na best practice tumefundishwa hukuhuku diaspora ni jukumu letu kujipanga na kuziundia mikakati ili tuachane na mijadala isiyotuhusu inayoendelea kwenye jamii zetu ikitokea kule nyumbani.

Tunapoteza muda mrefu kuongelea vitu vilivyoliwa tayari kama ESCROW,EPA N.K na tunaacha kujadili na kujua nini kimebaki ili tukitafute. Hizo kashfa hazitaisha kwani tuliowengi hatujui mali zipi ziko wapi mpaka zimeliwa ndo tunaamka na kujadili! Sasa si wakati huo kwa wana-diaspora tuanze kutafuta fursa zitakazotupelekea kuona mali zilizobaki ili tushiriki kuziendeleza kwa manufaa ya nchi yetu na vizazi vyetu.

Naomba nimalize kwa kusisitiza kuwa matawi ya nje ya ccm pamoja na;1. kulinda itikadi ya chama chetu,2. kutafuta wanachama wengi Zaidi, 3. kulinda taasisi za serikali kwenye diaspora husika, , kwa hapa ccmUK kwanza

tunajukumu la kuzilinda taasisi mbalimbai za serikali yetu kama ubalozi wetu Kwani sisi ni chama tawala kwa sasa. Na tunatakiwa kuitetea taasisi hiyo katika mfumo wake wa sasa huku tukiendeleza mawasiliano ya kitaasisi ya namna bora ya taasisi hiyo ya serikali inavyoweza kusaidiana na vikundi vingine vya kijamii na kiuchumi hapa UK katika kusaidia na hata kuwezesha watanzania ku-engage pro-cess za kuzitambua fursa mbalimbali zilizoko hapa na nyumbani ikiwa ni pamoja na kusaidia kuandaa forums mbalimbali.

4. kuandaa makada wenye muono mpana Zaidi ili waje kusaidia na kuongoza chama huko siku za mbeleni,

5. Pia lazima yawe chachu ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu na ndipo tutakapokuwa na uwezo wa kupima kwa kiasi gani tumefikia malengo ya kamati kuu ya kuanzishwa kwa matawi hayo.

Imetolewa na Abraham Sangiwa – Katibu wa Itakadi Siasa na Uenezi

CCM UK/01/2015

Page 12: MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CHAMA CHA MAPINDUZITAWI LA UNITED KINGDOM

Email [email protected] Tel+44 78 33571100.Website: www.ccmuk.org , blog: ccmuk.org/blog; Twitter - ccmuk1, Facebook & Facebook page; chama cha mapinduzi uingereza.

Chama Cha Mapinduzi – TAWI LA UINGEREZA (UNITED KINGDOM).

Makala hii inapatikana kwenye blog yetu CCMUK.ORG/BLOG

CCM UK/01/2015