9
Ijumaa Februari 22, 2012 KUWAUNGA MKONO WADAU WA MAPINDUZI YA RUKA JUU IMERUDI TENA [email protected] Wasiliana nasi bure kwa ujumbe mfupi kwenye simu andika KILIMO kwenda 15774 Ikiwaletea kwa mara nyingine fursa kwa maisha yote kwa vijana ...Ruka JUU, changamoto ya biashara kwa vijana, sasa imerudi tena. Ni kwa vijana juu ya Biashara Kilimo.

Nipashe Kilimo Kwanza issue number 48

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Nipashe Kilimo Kwanza issue number 48 SEND YOUR COMMENTS FOR FREE TO 15774 BY STARTING WITH THE WORD “KILIMO” FOLLOWED BY YOUR COMMENTS

Citation preview

AIjumaa Februari 22, 2012 KUWAUNGA MKONO WADAU WA MAPINDUZI YA

RUKA JUUIMERUDI TENA

[email protected] nasi bure kwa ujumbe mfupi kwenye simu andika KILIMO kwenda 15774

“ Ikiwaletea kwa mara nyingine fursa kwa maisha yote kwa vijana...Ruka JUU, changamoto ya biashara kwa vijana, sasa imerudi tena.Ni kwa vijana juu ya Biashara Kilimo.

Na Pendo Mashulano

“Nikiwa kinda la miaka mitatuna ‘vijino’vyangu vichache tukinywani, tayari nilishakuwa‘mkulima’ ”, anasema GeoffreyMartin Sadana, mwanafunziwa shule ya sekondari Nkasi,

mkoani Rukwa.“Katika kigizagiza cha kuelekea

pambazuko, mama alininyanyua kuto-ka kitandani, akanitupia mgongoni nakunifunga vizuri kwa mbeleko. Kishaalibeba jembe lake, tayari kwa safariya shamba kilometa kadhaa kutokanyumbani. Sikujua kilichokuwa ki-naendelea kwani ilikuwa usiku nalalakitandani lakini kila nilipoamka nili-jikuta shamba.”

“Tukiwa shamba nilichezea cho-chote kilichokuwa karibu nami,kuanzia udongo hadi mabua na mamahakunizuia, aliniacha nicheze, ilimradisikitu kinachoweza kunidhuru. Kwakutumia kijiti au jiwe lenye ncha, nili-

tifua ardhi na kupanda mbegu aumimea, kama nilivyokuwa nikionawazazi wangu wakifanya! Niliweza ku-jaza hata mahindi kumi kwenye shimomoja na kufukia, yalipoota kila mtu al-ijua ni mimi. Kwa ufupi, kilimo ki-likuwa ndiyo mchezo wangu wa uto-toni,”

“Nilipotimiza miaka mitano,wazazi wangu walinitengenezea jembela saizi yangu, nikaanza kusaidia kazindogondogo za shamba kama palizi,kuchimbia vitunguu na nyingine zanamna hiyo. Kadri miaka ilivyokwen-da ndivyo umaridadi wangu katika kil-imo ulivyoongezeka.”

“Nilipotimiza miaka saba nilikuwana uwezo wa kulima hadi yadi 6 x 20.Nilijifunza kilimo kwa kupiga mzigo,siyo kwa kutazama. Kadri miakailivyokwenda ndivyo uwezo wanguulivyoogezeka na kila baada ya mudawazazi wangu waliniongezea ukubwawa eneo la kulima; hivyo ndivyo

walivyonifundisha kazi. Nawashukurusana.”

“Tangu wakati huo, kilimo kikawandiyo maisha yangu, nikajua kwambani kutokana na kilimo tu napatachakula, elimu, mavazi, na mahitajiyote ya familia. Leo hii, japokuwa nikoshule, lazima niutafute muda wa ku-ungana na familia katika kazi zashamba, japo wikiendi na wakati walikizo,” Geoffrey anamalizia.

Bahati naye anasimuliaNdiyo! Ni dada Bahati Yule yule

wa Fema TV Talk Show. Ni ‘mkali’shambani kama alivyo ‘mkali’ kwenyeruninga, sikiliza simulizi yake.

“Wakati nakua, nakumbuka,shamba la familia lilikuwa ‘hatua’ ki-dogo kutoka nyumbani. Jogoo la kwan-za tu lilipowika, tulidamka, tukaoshanyuso zetu na chapchap tulikamatajembe tayari kwa safari ya shambapamoja na wazazi wetu.”

“Ukiacha shamba kubwa la famil-ia, tulikuwa na eneo kubwa mbele yanyumba yetu na yeyote katika familiaaliyetaka kulima pale aliruhusiwa.”

“Nilikuwa na kibustani changupale, nikilima mboga za majani –spinachi, ‘chainizi’, au kabichi. Mbogahizi zilikuwa zikitumika kwa msosi wafamilia lakini niliruhusiwa kuuza kiasina kutumia fedha kununua chochotenilichohitaji.”

“Kutokana na biashara hii ndogo,nilikuwa na pocket money yangu mudawote na nilikuwa na uwezo wa kujin-unulia pamba za ukweli wakatiwowote nilipohitaji. Wazazi wangu wa-likuwa wakijivunia sana juhudi zangu!Nani atathubutu kusema kilimo hak-ilipi?”

Simulizi zetu zinafanana mnoMuda wote ninapozungumza na

Geoffrey na Bahati kwa ajili ya makalahii, akili yangu inakumbuka mbaaaalisana. Nakumbuka enzi zileeee ‘mwaka

47’! ‘Yeah’, simulizi zangu zinafananamno na simulizi za maisha yangu.Hata ukiniuliza ni lini haswa nilianzakujihusisha na kilimo, nitakwambiaSIJUI. Nilipata akili nikajikuta tayarinakwenda shamba na watu wote kati-ka familia yetu!

Nimezaliwa na kukulia katika fa-milia yenye watu wengi na ilipotimusaa ya shamba wagonjwa na watotowachanga tu ndio ‘waliosamehewa’!Hata tulipokuwa tumeshatawanyikakatika shule mbalimbali za bweni –wakati wa likizo kila mmoja alitenge-wa ‘pande’ lake na aliyemalizaaliruhusiwa kuorodhesha mahitajiyake ya shule na kupewa fedha.

Kilimo kilikuwa ndiyo mpango mz-ima na hakuna aliyelalamika wala ku-sononeka! Tulikuwa tukifahamu fikakwamba mahitaji yetu yote – kuanziaada za shule hadi msosi – yalipatikanashamba.Tulifahamu pia kwamba sisindiyo nguvukazi ambayo wazazi wetuwalijivunia na kuitegemea na kamatusingeifanya kazi hiyo hakuna mtuyeyote ambaye angekuja kuifanya kwaniaba yetu. Nilikuwa nikifanya kazi‘usiku na mchana’ ili nimalize kipandechangu mapema, nipate japo sikuchache za kutembelea ndugu na jamaakabla ya kurudi shule. Maisha yalien-delea kwa mtindo huo mpaka wotetukahitimu masomo yetu.

Leo hii, tumetawanyika sehemumbalimbali nchini, tukifanya kazi to-fauti – wengine ofisini, wengine sham-ba na wengine kotekote! Waliochaguakuendelea na kilimo, uzoefu wao wautotoni umewasaidia kuifanya kazihiyo vizuri sana na wamekuwawakulima bomba vibaya mno!

‘Ukinitupa’ shambani leo hii,hutoamini kwamba ndiye yuleyulePendo Mashulano, unayemsoma kilaleo katika Fema! Sina ugeni wowotekatika anga hizo, utashangaa!Nashukuru sana kwa uzoefu nilioupa-ta wakati na kua kwa nini na ujuzi waziada ambao naweza kuutumia wakatiwowote!!

Wewe je? Baadhi yenu wanafunzi tayari

mnajishughulisha na kilimo, lakiniwengine pengine hamjawahi hata ku-gusa jembe. Sawa? Je, unafahamukwamba kilimo ni maisha? – kila kitu,kuanzia ada ya shule, ‘vocha’ za simu,nguo na chakula, vyote vinatoka sham-ba! Je, umewahi kufikiria kulima ki-jishamba chako mwenyewe? Unawezakupata mshiko wa ziada na kuchangiakatika ‘pocket money’ yako kama alivy-ofanya Dada Bahati enzi zake! Je, ume-wahi kujiuliza ni kiasi gani cha fedhaunaweza ‘kutengeneza’ kwa kulimajapo eneo dogo tu la mbogamboga?

Tafakari na uanze sasa! Kuwamjanja! Kilimokinalipa!

Kumbuka:Kujishughulisha na kilimo wakati

ukiwa masomoni kutakupatia wewe nafamilia yako kipato cha ziada. Tumiamuda wako wa jioni, ‘wikiendi’ nawakati wa likizo kwa kulima na uki-fanye kilimo kuwa sehemu ya maishayako. KUMBUKA, chakula, vitabu,nguo, ada ya shule na hata ‘pocketmoney’ –vyote vinatoka shamba.Baadaye katika maisha yako, unawezaukawekeza zaidi katika kilimo nakutengeneza faida kubwa kibiashara.KUNA FURSA ZA MAANA KATIKAKILIMO!!!

3MAISHA2 UJUMBE WETUIjumaa Februari 22, 2013 Ijumaa Februari 22, 2013

NDANI

TANZANIA inakabiliwa na tatizo laajira katika sekta rasmi, umaskinikwa wananchi wake na upungufuwa chakula katika baadhi ya mae-neo.

Baadhi ya vijana wenye nguvu za kutoshawamekuwa wakirandaranda mitaani na kukaavijiweni mijini na vijijini kwa kile kinachodai-wa kuwa hawana shughuli za kufanya.

Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbalikuanzia ngazi ya vyeti hadi shahada,wanahitimu kila mwaka na kujikuta waki-hangaika kutafuta ajira katika sekta rasmihuku wengi wao hawafanikiwi kwa sababu yaufinyu wa nafasi hizo.

Kundi la watu hao ambao ni nguvu kazimuhimu kwa taifa, baadhi yao hujikuta wak-izurura au kufanya shughuli ambazo hazinatija au zile za bora mkono uende kinywani.Hawaboreshi maisha yao, kuchangia pato la fa-milia na uchumi wa taifa.

Ushahidi uko wazi kuwa wakati mwinginevipaumbele vyetu havielekezwi katika maeneosahihi. Kwamba wapi tuanze na wapi tumal-izie.

Mathalani, katika eneo la kilimo, maelezo

na mipango mingi imekuwa ikielezwa kuwainalenga kubadilisha kilimo chetu kutoka jembela mkono ambalo limekuwa linatumiwa nawakulima wengi kwa mikoa mingi na kuelekeakatika kilimo cha kisasa chenye tija.

Kaulimbiu mbalimbali zimekuwa zikitole-wa kutoka Siasa ni Kilimo hadi Kilimo Kwanza,lakini mapinduzi ya kilimo yamekuwa yak-ibadilika kwa kasi ndogo sana.

Kilimo kinaelezwa kuwa ni uti wa mgongowa taifa na kinaajiri zaidi ya asilimia 80 yaWatanzania ambao wanaishi vijijini. Kwa hiyoeneo hili linatakiwa kupewa kipaumbele chauhakika ili kuleta mapinduzi ya kweli nakuwafanya wakulima waongeze uzalishaji,kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na bi-ashara, kuongeza usalama wa chakula nakupunguza kiwango cha umaskini kinachowak-abili watu wengi.

Haiaminiki hata kidogo leo hii kusikiabaadhi ya maeneo yakiwamo yale yanay-opakana na maziwa na mito, watu wanaishikwa kula mlo mmoja huku wakikabiliwa naumaskini wa kiwango cha kutisha.

Kilimo cha umwagiliaji kimekuwa kinata-jwa kuwa kitasaidia sana kutuondoa katikautegemezi wa mvua ambazo miaka ya hivi kari-

buni, mvua zimekuwa hazitabiriki sana kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi na kus-ababisha hasara kubwa kwa wakulima nakushusha kiwango cha uzalishaji wa mazao yaaina mbalimbali.

Tunaweza kulima kilimo cha uhakika kwasababu ya neema ya maji tuliyonayo kwasababu nchi imezungukwa na mito, mabwawana maeneo nyevu nyevu mengi karibu kila konaya nchi.

Hata hivyo, utekelezaji bado hauendi kwakasi inayozungumzwa. Kwa hiyo, tunatakiwakupima kwa makini vipaumbele vyetu nauwekezaji ili kuhakikisha kuwa nguvu kazi yavijana tuliyonayo inatumika kuzalisha kwa tijana kutuondoa hapa tulipo.

Matumizi ya teknolojia rahisi na mitambokama itapatikana kwa urahisi ni kwamba kil-imo kitavutia vijana na watu wengi kwa sababuya faida inayotarajiwa kupatikana.

Wakati unapopitishwa uamuzi wakutekelezwa Kilimo Kwanza ili kuinua uzal-ishaji na kuleta mapinduzi katika kilimo, yali-ingizwa matrekta na baadhi ya mitambo .

Tuna ardhi kubwa yenye rutuba na uhaki-ka wa soko la chakula ni mkubwa hata katika

nchi jirani za Afrika Mashariki na kwingineko.Kinachotakiwa ni kutoa mikopo yenye riba ndo-go kama ilivyosemwa kuwa itaanzishwa benkiya kilimo, inatakiwa ionekane kweli ni tegemola wakulima.

Hali kadhalika, ufugaji mdogo mdogo kamawa kuku, nyuki na mwingineo, unaoweza ku-fanywa na watu wengi kwa mtaji mdogo, nimuhimu ukahimizwa na kuhamasishwa vilivyo.

Pia kilimo cha mazao mchanganyiko ya bus-tani ikiwamo mboga mboga, matunda na mauakwa wakulima wanaofanya miradi hiyo,umechangia mabadiliko ya kuboresha maishana kuchangia pato la familia na taifa kwa ujum-la.

Jesse KwayuMhariri

Ardhi itumike kuvutiavijana kujiajiri

4

Tatizo la ufugaji wanyamana mabadiliko ya tabia nchi

15

Umoja ni nguvu!

7

Bustani: Rasilimali kubwa,fursa nyingi

Kilimo Kinalipa

Tuma maoni yako bureukianza na neno LIFEkwenda namba 15774

Mkurugenzi Mtendajiwa Chama cha BustaniTanzania (Taha) ,Jacqueline Mkindianazungumzia masualambalimbali ikiwamomipango, mikakati nauwekezaji katika sektahiyo kamaalivyofanyiwamahojiano naMwandishi wa KilimoKwanza:

SWALI: Je kuna aina gani yakuwapo fursa za uwekezaji katikauzalishaji wa kilimo cha bustani?Je, wanaweza kuzungumziamahitaji ya masoko?

JIBU: Uzalishaji wa matunda namboga kwa ajili ya masoko ya ndanina Kimataifa katika Tanzania ni yachini sana ikilinganishwa na rasilimaliinayopatikana kwa uzalishaji nchini.Mahitaji ya soko ya mboga zenyethamani yapo juu (kijani maharage,mbaazi, mtoto mboga, pilipili ) namatunda kama vile maembe, avocadosna mananasi yamekuwa yakiongeze-ka.

Kujenga mazingira mazuri ya ku-vutia wawekezaji ili wawekeze katikasekta ya maua, TAHA imekuwa iki-fanya kazi kwa karibu na serikalikuhusu masuala kadhaa kama vilekuhamasisha wakulima wadogo na wakati wa kuzalisha na huduma ya mahi-taji ya soko.

Pamoja na wakulima wadogo,TAHA ina jukumu la kuhamasisha nakujenga uwezo wa wakulima hawa nakuunganisha na wanunuzi au makan-darasi, kutoa mafunzo juu ya kuzinga-tia viwango kwa ajili ya kukabilianana ushindani katika soko.

Hivi karibuni, TAHA ilitambuliwamwekezaji aliyekuja kuwekeza katikasoko la nje la mboga na mpango wa ku-nunua hadi tani 100 za mboga ya kilasiku ili kuongeza mauzo ya nje na ik-ilinganishwa na hali ya sasa yawastani wa tani 50 kwa siku.

Ingawa mwekezaji huyu

5

A

BUSTANI4

A

BUSTANIIjumaa Februari 22, 2013 Ijumaa Februari 22, 2013

Bustani: Rasilimali kubwa, fursa nyingi

anaelekeza nguvu katika eneo laKaskazini (Kilimanjaro, Arusha,Manyara na Singida).Kuna wawekeza-ji wengine ambao wanalenga mikoamingine.

TAHA imekuwa ikifanya kampeniya kuhamasisha wakulima wadogo nawa kati ukubwa kuzalisha kwa ajili yakukabili soko hili.

SWALI: Kwa kifupi unawezakueleza hatua za mkakati, mbinuza uzalishaji, viwango, kuongezathamani na upatikanaji wa ma-soko kwa ajili ya wazalishaji wamananasi?

JIBU: Upatikanaji wa masokoumekuwa kikwazo kwa wakulima wabustani katika sehemu mbalimbali zanchi kutokana na miundo mbinu duni,vifaa na uwezekano wa kupata fedha.Moja ya malengo ya TAHA ni kuimar-isha uhusiano kati ya mnunuzi namuuzaji.

Moja ya malengo ya mchakato huomwaka huu ni kuwaunga nisha wazal-ishaji wa Chama cha WazalishajiMananasi wa Kiwangwa (KIPA) nawenzao kutoka kanda ya Ghuba, am-bao wako tayari kununua kontena tanokwa wiki kutoka kwa wakulima hao.

Taha itaendelea kuhamasishawakulima kuhakikisha wanatumiateknolojia sahihi. Chama pia ki-nafanyia kazi kuhakikisha kiwangocha uzalishaji kinaongezeka, aina, naviwango vya kuendeleza soko hili.

SWALI: Je, una mkakati waUshirikiano kuhakikishakuongeza uwezo katika sekta ndo-go ya kilimo cha mazao ya bustani,mboga na matunda?

JIBU: TAHA ina dhamana ya ku-panua huduma zake kwa kuwafikiawakulima wa mazao ya bustani, mbogana matunda na wadau wengine ikiwapamoja na kutoa msukumo kwa ku-lenga katika masoko ya kilimo katikakanda kwa kutumia majukwaa mbal-imbali.

Jukumu la TAHA ni kuongezauwezo wa wakulima ili wawezekushiriki kwa ufanisi na kuwa nauhusiano endelevu. Ili kufanikishahilo, TAHA imekuwa ikishiriki katikaubia na mashirika mbalimbali ya ki-taifa na kimataifa ili kuhakikishakwamba huduma za msaada wa bi-ashara unatolewa kwa sekta.

Ni kwa suala hili kuwa chama wal-iungana na Kilimo Trust, ili kufanyakazi pamoja na kutambua usalamawa chakula na kuongeza mchango wakilimo ili kutokomeza umaskini, kama

vile kuongeza tija na faida za kampuniza biashara ndogo.

TAHA na Kilimo Trust wametiasaini makubaliano ya kushiriki katikajuhudi za pamoja ili kuhakikishaongezeko la tija na ushirikiano wa sek-ta ndogo ya mazao ya bustani nambogamboga nchini Tanzania katikakanda na mnyororo wa dunia.

Tunafanya hivyo kwa kutumia fai-da ya fursa kubwa ya ardhi nchini narasilimali za ardhi na maji kufikiahatua kuelekea kwa muuzaji nje wamazao ya kilimo.

SWALI: Unaelezeaje namnamnavyojipanga kuanzisha mafun-zo ya vitendo kuhusu kilimo chabustani katika kituo cha ubora(PTC)? Unadhani itafanikiwa ?Kwa namna gani?

JIBU: TAHA imetia sainimakubaliano na serikali kupitiaWizara ya Kilimo, Chakula naUshirika Aprili 2012, ardhi imetengwakwa ajili ya kuanzisha kituo cha ku-jitegemea cha ubora kwa mafunzo yabustani kwa vitendo (PTC).

PTC watakuwa wanatoa mafunzokwa maeneo mbalimbali ya mnyororowa uzalishaji wa mazao ya bustani,maua na matunda, mbinu bora zakisasa na huduma nyingine za msaadawa kiufundi kwa wakulima.

Kwa sasa , TAHA hutoa mafunzojuu ya mbinu bora za kilimo, kilimokama mbinu ya biashara, uvunaji nabaada ya mavuno, miongoni mwawengine.

Kwa hiyo, TAHA inasukuma gu-rudumu, lakini badala ya kutumia ki-tuo cha mafunzo kuimarisha mafunzoya sasa na kuwa na "maabara" namchakato mzima wa mnyororo wathamani.

PTC itakuwa chombo endelevu navyombo sahihi binafsi na serikaliwakati wa kudumisha dhamira yakekwa wakulima wa bustani . TAHAimeanzisha mfululizo wa shughuli nakuanza utekelezaji wa mradi huu.

Maendeleo ya kituo hiki itakuwakwa awamu. Awamu ya kwanzaitahusisha ujenzi wa majengo, mbogamboga kwa vitendo na viwanja vyambegu na kisha shamba vitendo / vi-wanja kwa ajili ya matunda . Wakatiawamu ya tatu itahusisha maendeleoya mashamba kwa ajili ya maua maua.

Tuma maoni yako bure ukianzana neno HORTICULTUREkwenda namba 15774

7

A

UMOJA6

A

TABIAIjumaa Februari 22, 2013 Ijumaa Februari 22, 2013

Na Gaure Mdee

“Mama alifariki nikiwa na umriwa miaka 17. Hii ilikuwa ni mi-aka sita baada ya baba kufariki,wakati huo nikiwa ndiyo kwan-za nimehitimu darasa la sabahuku mdogo wangu wa kike

akiwa darasa la nne. “Hatukuwa na chanzo cha mapato

na nilihitaji kumaliza kidato cha nnekwa namna yoyote ile. Tulikuwa nahekari tatu za shamba na sikuwa nauhakika wa kulifanyia nini shambahilo au nitalitumiaje,” anafafanuamkulima Frank Kalezi.

Kwa sasa Frank ana miaka 32,mke na watoto watatu. Alilitumiashamba hilo kwa kilimo akiwa na dadayake na watoto wake wawili.Alilitumia kupata faida ya ziada.

“Changamoto nilizokutana nazowakati ule na ninazokutana nazo sasazinafanana. Kwa kifupi nawekamkakati na nakabiliana nazo tofautisasa. Nilifanikiwa kupitia kujitambua,bahati na msaada kutoka kwa maofisakilimo,” anasema.

Kwa wanaojipanga kuingiakwenye kilimo ili kupata faida siku fu-lani au wale ambao tayari tunafanyashughuli hiyo itakuwa ni busara kuzin-gatia ushauri huu. Jiandae.

Zifuatazo ni mbinu za kukabilianana changamoto zinazoweza kujitokezakatika kilimo.

Changamoto: Mtazamo hasikuhusu kilimo

Watu wengi wanakatishwa tamaana hali ya unyanyapaa kuhusu kilimo.Tunasikia watu wakisema “Kilimo niuchafu, ni kwa watu masikini na wa-sio na elimu!”

Hata katika shindano la BongoStar Search baadhi ya majajiwanawakatisha tamaa washiriki kwakuwaambia warudi shamba kamakwamba kilimo ni kitu cha kutia aibu.Mawazo haya yako mbali mno na uk-weli. Hakuna kitu cha aibu ukiwamkulima mjanja na unayejiongezeakipato kihalali.

Frank anasema “tabia hii in-apoteza dhana ya kilimo kwenye taifahili” Inafanya vijana wengi kukipamgongo kilimo na kuona kama sishughuli ya maana kwao, mwishowake wanajikuta wamepotea.

SuluhishoKilimo kina thamani na kinaweza

kuwa sekta yenye faida kubwa kwasababu watu wanahitaji kula, soko labidhaa za kilimo linakuwapo kilawakati hususani mazao ya chakula.

Kila sekta inalipa kwa wale tu am-bao hujitoa na kufanya kazi kwa bidiina ndiyo ilivyo hata kwenye kilimo.Hivyo usiogope jembe kwa sababu kil-imo ni fedha. Kifanye kuwa shughuliyako rasmi.

Changamoto: Ukosefu wa ufa-hamu na maarifa

Wakulima wengi wanakosa maari-fa ya kukipeleka kilimo katika hatuanyingine. Wanaridhika mara tuwanapopata fedha kidogo.

Frank alitaka msaada wa OfisaUgani aliyemfundisha jinsi ya kulimakwa faida. Aliuza magunia manane ya

mahindi kwa mara ya kwanza na ku-nunua hekari nyingine, “…baada yakupata hekari nyingine nilijikutaghafla nimeanza kupata fedha nyingi,na nilihakikisha kwamba nawezakumsomesha dada yangu.”

Suluhisho:• Kila kijiji kiwe na fursa ya kupata

ushauri wa bwana au bibi shambakatika eneo lao. Hawa wanautaalamu wa kuelewa ni zao lipilinalofaa zaidi katika eneo husika,aina gani ya mbolea na viuatilifuutumie shambani kwako. Kazi yao

ni kusaidia wakulima na una hakiya kupata msaada wao.

• Tafuta makundi ya kilimo katikajamii unayoishi ambako pamojamtabadilishana mawazo nakushauriana juu ya kilimo. Kamahakuna shirikiana na jirani yakokuanzisha kikundi. Umoja ni ngu-vu!

Changamoto: Upungufu waPembejeo

Mbolea na mbegu wakatimwingine hutolewa na serikali kupitiaruzuku; hata hivyo hufika zikiwa

zimechelewa.

Suluhisho: • Jinunulie mbolea yako. Frank

kamwe hakusubiri ruzuku ya pem-bejeo; huenda na kununuamwenyewe.

• Uliza katika kundi la wakulimawenzio au kwa bwana au bibishamba juu ya mazingira yako.Fahamu muda mzuri wa kupandaili kuepuka wadudu waharibifu najinsi ya kujitengenezea mboji.“Mazao yanakuwa imara zaidikuhimili mashambulizi ya wadudu

kama utapanda kabla ya kipindicha unyevunyevu,” anasemaFrank.

• Katika kundi lako, wanachamawanaweza kufuata pembejeo kwamawakala wilayani au mkoani.Kama mtakumbushana mara kwamara mambo yanawezakutekelezwa mapema.

Changamoto: Ukosefu wa sehe-mu za kuhifadhi mazao

Uhifadhi na uchakataji wa mazaoni njia nzuri ya kuongeza thamani yamazao yako; hasa kama unasubiri hadibei ya zao iongezeke sokoni, na hapoutapata bei nzuri.

Suluhisho: • Frank alikua anatunza mazao

yake uvunguni na sebuleni, kituambacho mkewe alikuwa hapendi.Baadaye, alipata nafasi ya kuhi-fadhi ghalani.

• Watu katika vyama vya wakulimahuweza kupata sehemu ya kuhi-fadhia mazao au mnaweza kupun-guza gharama za kusafirishamazao kwa ajili ya kupeleka gha-lani.

• Pia mbinu zaidi za kijadi katikauhifadhi wa mazao kama vileVihenge hutumika kuokoa jahazi.

Changamoto: Uhaba wa masokoKutafuta soko la bidhaa zako ku-

naweza kuwa changamoto kubwa, um-bali kutoka shambani hadi sokoni auwakati mwingine kutopata kile una-chohitaji.

Frank huhakikisha kwamba kilaanapokwenda sokoni tayari anakuwana wateja wa kuwauzia mazao yake nakama mnunuzi hajaridhika na beianayotaka basi huamua kufanyauchakataji kwa kusaga mahindi kuwaunga na kisha kuuza kwa watu kwa beinzuri zaidi.

Suluhisho: • Panga kabla: Jadiliana kuhusu bei

na fanya makubaliano ya bei namteja wako au dalali kabla ya kuu-fikisha mzigo.

• Kuwa na mkakati mbadala: Kamamnunuzi hakubaliani na bei yako,peleka biashara yako sehemunyingine au tafuta njia nyingine yakuuza bidhaa zako.

• Ni vyema kuanzisha chama ilimuweze kujadiliana na kupata beinzuri ya pamoja.

Kumbuka.Kilimo ni kazi yenye changamoto

kama zilivyo kazi nyingine. Unawezakupata fedha nzuri na kupatamafanikio kama utajituma nakuongeza bidii kutatua changamoto zi-nazojitokeza. Hata hivyo kama ilivyokwa kazi zingine unahitaji vitu vitatu –Uvumilivu, Mipango na Nia ya dhati ilikufikia kileleni. Kuwa mjanja, jipange!Nenda..chukua jembe, ondoka kivuliniuende shamba.

Jishughulisheshambani ufanikiwe

Na Gaure Mdee

Hapo zamani za kale pa-likuwapo na joka kub-wa. Viumbe wadogo,wadogo waliliwa hadilikanenepa sana, kiasicha kushindwa kuenea

katika shino lake. Hivyo likalazimikakutafuta shimo jingine.

Joka lilifika katika kichuguu chasiafu na kusema “Mimi ni nyoka ninanguvu sana nipisheni katika shimohili nataka kuishi hapa.”

Siafu wakasema “Tumewekezanguvu nyingi kujenga mji wetu, tu-taondokaje?” Joka likasisitiza lazimawaondoke likiwa na uhakika kuwa sia-fu kwa udogo wao hawawezi kumfanyakitu.

Alikosea. Siafu wakatambua ud-haifu wao, ila wakapanga mpango,“Tushirikiane wote kwa pamoja” wali-nong’onezana. Wote wakapandakwenye mwili wa joka lile, na maramoja wakaenea mwili mzima.Wakaanza kuliuma. Joka kuona vilelikashindwa kuvumilia maumivu nakukimbia ili kuokoa maisha yake. Kwaumoja, siafu wadogo, wakafanikiwakulishinda joka kubwa.

Pamoja mnawezaKama walivyo Siafu, wakulima

walioungana huwa na nguvu na uwezowa kukabiliana na changamoto ngu-mu.

Mfano halisi ni wakulima wa miwawa huko Mtibwa. Mwaka janawalipoona wanalipishwa kodiwasiyostahili, kwa kutumia Chamacha Wazalishaji Miwa Mtibwa ( MOA),kilichukua hatua ya kwenda Baraza la

Kilimo Tanzania (ACT) kutafuta msaa-da.

“Tuliwaambia ACT kwambawakulima wa Kilombero wanalipa kodikidogo kuliko sisi katika mzigo wa ainamoja wa miwa. Hii siyo haki kwetu.ACT walilichukua suala hili na kulifik-isha serikalini. Waziri Mkuu aliagizakodi hizo zirekebishwe, nasi tukapatamsamaha,” anasema Hadija Kondo,Mwenyekiti wa MOA.

Unganisheni nguvu kwa faidaya wote

Kujiunga katika klabu, vyama aumakundi kuna manufaa mengi. Nakama hutuamini basi shika haya kuto-ka kwa Mbunge anayetushirikishauzoefu wa jambo hili.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe, anasema pembejeo za kil-imo zilichelewa sana mwaka uliopitana kuhakikisha kuwa zinafika mape-ma msimu unaofuta kwa kuwapaushauri wakulima jimboni kwake.

“Niliwaambia waungane na waji-pange vizuri. Hakuna njia mbadalakatika hili. Mnahitaji kuungana katikakundi kubwa, na kama kungekuwa nashida niliwashauri pia wawahusishewaandishi wa habari kamawanaweza.”

Ushauri wa Zitto unajidhihirishakuwa na manufaa katika mfano ufu-atao.

Kikundi cha walikuma chawanawake kilichojipanga vizuri hukoIjombe mapema mwaka jana, walijiku-ta katika wakati mgumu baada yakuambiwa kwamba ardhi waliyokuwawakilima kwa miaka yote si mali yaotena.

“Viongozi wa kijiji walikodishaardhi kwa watu wengine na kuchukuafedha katika mchakato huu. Tuliendakuomba msaada kwenye Kituo chaMsaada wa Kisheria na Haki zaBinadamu (LHRC) kituo cha Mbeya.Walikuja na waandishi wa habariwalioripoti suala hili na kuwapakashkash viongozi wa kijiji na hati-maye waliturejeshea ardhi yetu,”anasema Salome Simon, Mwenyekitiwa kikundi cha wanawake wakulimacha Ijombe, mkoani Mbeya.

Pengine hili lisingetokea bila ngu-vu na nia ya dhati ya kina mama wale,na msaada kidogo kutoka kwa Diwanialiyehakikisha kuwa anakutana na

viongozi wa kijiji. Mfano wa uongozibora ulionekana. “Fedha zilizochukuli-wa kutokana na kukodishwa ardhi yaozilirejeshwa na kupelekwa kufanyakazi ya ukarabati wa shule,” anasemaSaid Mohamed Mwenyekiti wa Kituocha Sheria na Haki za Binadamu,Mbeya.

Manufaa ya kujiunga na vikundi!

• Gharama ndogo za uendeshaji:Kama kikundi mnaweza kununuapembejeo kwa pamoja. Mara nyin-gi pembejeo huuzwa kwa punguzomaalum na hivyo mnawezakuchangia gharama za usafirishajina hivyo kujiongezea faida! KuwaMjanja!

• Nguvu zaidi ya kupanga bei:Kukabiliana na madalaliwanaopandisha na kushusha beikiholela inaweza kuwa rahisikama wakulima mtakuwa wamojawenye sauti ya pamoja. Kamakikundi mnaweza kupanga bei nakulazimisha ikubalike. Tumieninguvu yenu!

• Kutenda pamoja (kama siafu):Umoja ni nguvu. Kama mna tatizoau mnadhani mmefanyiwa visivyo,msikae kimya, unganisheni nguvuna mzungumze kwa sauti moja.Pamoja mtashinda.

• Kufanya maamuzi ya pamoja:Kuwa katika kikundi ku-nawafanya kujifunza na kupatambinu bora za kilimo. Piamtafanya maamuzi mazuri juu yamasuala yanayowaathiri wakuli-ma wote.

• Mtaonekana: Serikali za mtaa aukijiji na asasi binafsi zikitambua

uwapo wenu mara nyingi ni rahisikusaidia makundi kuliko mtummoja mmoja. Kifanyeni chamaau kikundi chenu kifahamike.Manufaa mengine ni kwamba un-

akuwa na kazi chache za kufanyamnapofanya kazi pamoja!

Changamoto hazitakosekanaWakati mwingine kuna watu huta-

ka kuwa vinara, msiruhusu hili litokeekatika kundi lenu. Msiruhusu mtummoja kutumia mwanya huo kwamanufaa binafsi au kuwa na nguvu ku-liko wengine.

Wekeni mambo wazi kadri inavy-owezekana na hakikisheni kila mmojaanawajibika.

Ndiyo, mtu yeyote anaweza ku-jaribu kukimbia na fedha hivyo

• Kuweni makini na uchaguzi wawanakikundi, si kila mtu nimwaminifu.

• Kuweni na uvumilivu; Kwa kwelimnatakiwa kuwa na uvumilivu wahali ya juu kwa kila mmoja.

• Ikiwezekana muwe na katiba aumuweke sheria zitakazoliongozakundi lenu ambazo kila mwanakikundi atalazimika kuzifuata. - Muheshimiane, bila hivyo

mambo hayatasonga.SEMA NA FEMA. Kwa uzoefu

wako kuunda kikundi au klabu kunafaida? NDIYO, HAPANA? Tuandikiena utuambie kwa nini?

“Niliwaambiawaungane nawajipange vizuri.Hakuna njia mbadalakatika hili. Mnahitajikuungana katikakundi kubwa, nakama kungekuwa nashida niliwashauri piawawahusishewaandishi wa habarikama wanaweza

Umoja ni nguvu!

Tuma maoni yako bureukianza na neno DIGkwenda namba 15774

Tuma maoni yako bureukianza na neno FORCESkwenda namba 15774

9

A

HABARI YA MBELEIjumaa Februari 22, 2013

8

A

HABARI YA MBELEIjumaa Februari 22, 2013

Na Rebeca Gyumi

Unakumbuka shindanola ujasiriamali la RukaJuu kwenye runingamwaka 2011 lilikutan-isha vijana machacharisita walioshindania

nafasi ya kubadili maisha yao? Nishindano ambalo kinyozi kutokaKibaha, Idrissa Mannah aliibuka kid-edea? Sasa sikia, habari ya mjini ndiyohii, shindano la Ruka Juu limeruditena…na sasa ni kuhusu vijanawanaofanya kilimo kibiashara zaidi.

Kilimo ni bomba! Tumetembeleavijana makini wajasiriamali nchi nzi-ma wanaotumia kilimo kujengamaisha yao. Kila mtu anahitaji ajiraitakayomletea kipato, ila fursa za ajirazinaweza kuwa ngumu kupatikana.

Wakati fursa za ajira katika sektanyingine zinaweza kuwa chache, kil-imo kina fursa kibao kwa vijana.Kilimo cha kisasa ni muhimu, kamakijana mmoja anavyosema “ udongounanukia pesa, sema watu hawaonitu”.

Femina tunataka kukusaidia ku-gundua fursa iliyojificha kwenye kil-imo, usije ukapitwa kwa kilimo ki-naweza badili maisha yako.

Shindano la kwenye runinga RukaJuu limerudi, na msimu huu pia tunakipindi cha radio, Fema Radio, am-bavyo vitakwenda sambamba. Kwahiyo usikose kuangalia TV na kusik-iliza radio yako, upate ujanja wa kil-imo.

Timu ya Ruka JuuAmabalis a.k.a ABC: Ulimpenda

mtangazaji wetu mchangamfu kwenyemsimu wa kwanza, utampenda zaidikatika msimu huu wa pili. Muda huuanakuja amekamilika na maujanja yashamba. ABC atatuonesha njia na ku-tuthibitishia kuwa kilimo ni bomba.

Bwana Ishi: Hautamani kujuaBwana Ishi anatafuta nini shambani?Haswaa, mchekeshaji Bwana Ishianaingia kwenye kilimo, atakutana nasiri na changamoto za kilimo, usikosekuangalia.

Dada Bahati: Washiriki nawatazamaji wa msimu wa pili waRuka Juu wote wana nafasi ya kushin-da. Wasiliana na Bahati, ubahatike.Tuna majaji katika kila kipindi chaRuka Juu cha kwenye runinga, lakiniwewe pia uliyeko nyumbani unawezakupiga kura na kura yako ni muhimu.

Rebeca: Ulimuona Rebeca aki-tangaza kipindi cha Fema TV Talkshow, akiwa na ABC. Sasa utamsikiakwenye radio atakua mtangazajimwenza wa Fema Radio.

Michael Baruti: Unawezaukakumbuka sauti yake maridhawa,nzito kidogo wakati akifanya kazikama mtangazaji wa East Africa radio.Msubirie Michael, sasa ana-mix kwamtindo wa Fema.

Pia utakutana na vijana wengiwakulima na wataalam kutoka pandembalimbali za Tanzania wanaoishi nakufurahia zawadi ya ardhi. Kwa timuhiyo machachari usikose kufuatilia

Ruka JUU Imerudi TenaRuka Juu II, itakupagawisha.

Kwa nini Kilimo?

• Kilimo ni maisha: chakula kinajen-ga miili yetu, kinatupa nguvu. Kwakutumia chakula tunakuwa, tu-nakidhi njaa zetu, tunaponyamagonjwa mbalimbali. Tupotulivyo kwa sababu ya chakula.

• Kilimo ni utajiri: Kila mtu ni lazi-ma ale ili aishi kwa hiyo soko la kil-imo haliishi na hivyo basi hakunakazi nyingine yenye umuhimu ku-liko kilimo. Lima kwa usahihi naubora, kuna pesa ya uhakikakwenye kilimo.

• Ardhi kubwa yenye rutuba: Nchiyetu imebarikiwa ardhi yenye fur-sa kibao za kuendeleza kilimo.Wakulima wajanja wanaofahamunini cha kufanya kubadilisha ardhihii kuwa pesa.

• Kilimo ni uti wa mgongo:Unafahamu kuwa asilimia 85 yaWatanzania wanaishi kwa kutege-

mea ardhi. Nchi hii inategemea kil-imo. Sasa ni muda muafaka wotetuweke msisitizo kwenye kilimo nakukifanya kiwe na faida zaidi.

• Kilimo Bomba! Unaweza kuita kil-imo bomba au Kilimo Kwanza,kama kampeni inayoendeshwa naserikali. Tuungane wote na kukipakilimo kipaumbele. Tulishe kizazikijacho, tujenge maisha yetu.

Tumetembea, tukajifunza,tukafurahi

‘Tembea uone’ni msemo waKiswahili wenye maana, ukitembeaunajifunza mambo mengi. Na ndivyoilivyotokea kwa timu ya msimu wa piliwa Ruka Juu wakati wakitafutawashiriki katika mikoa ya Arusha,Morogoro na Rukwa.

Kutoka kwenye barabara korofi yaRukwa mpaka zenye vumbi ya Karatutimu ya msimu wa pili wa Ruka Juuilikutana na vijana wengi wakulima

(miaka 18 – 30), wakiendesha maishayao na wale wawapendao kwa kutumiakilimo. Timu imechagua wakulima

sita kutoka Monduli, Karatu, Kilosa,Mvomero, Sumbawanga na Nkasi am-bao watashiriki katika shindano laruninga. Tutakutana na wengi zaidikupitia kipindi cha radio.

Shindano la TVWashiriki ambao kwa sasa wanali-

ma mazao mbalimbali ya chakula kwaajili ya kujiingizia kipato, watawekastadi zao za kilimo na ujasiriamalikwenye majaribio watakapokuwawanapewa changamoto za shamba.Vipindi vimerekodiwa katika mazingi-ra ya kawaida ya washiriki.

Utakutana na familia zao, marafi-ki, kuangalia uwezo wao wa ushiriki napia utashiriki katika kuchagua mshin-di. Utaona jinsi shamba, linavyomtoaushamba mtu wa shamba. Na zaidi yayote utapata mawazo mapya kuhusukilimo.

UsikoseUngana nasi kwenye msimu wa

pili wa Ruka Juu! Angalia, piga kura,na jifunze kwa kiasi gani kilimo borakinabadilisha maisha ya vijana nchiniTanzania. Kilimo ni bomba, na tu-nasikia harufu ya pesa kwenye kilimo.

Ruka Juu ni nini?Ruka Juu ni moja ya zao la Femina

lenye lengo la kuhamasisha upatikana-ji wa ajira na kipato. Kwenye runinga,Ruka Juu ni shindano la ujasiriamalilinatumia maisha halisi. Msimu wakwanza ulionyeshwa mwaka 2011, nakutokana na maoni yenu ulifurahishasana.

Wengi wenu mlituomba tuendeleena vipindi na kuongelea vijana na kil-imo cha biashara. Kwa hiyo 2013Machi tutazindua msimu mpya, wekamacho na masikio yako wazi.

“Wengi wenumlituomba tuendeleena vipindi nakuongelea vijana nakilimo cha biashara.Kwa hiyo 2013 Machitutazindua msimumpya, weka machona masikio yako wazi

Tuma maoni yako bureukianza na neno BUSINESSkwenda namba 15774

Na Mwandishi Maalum, Ansaf

Kuboreshwa soko namsingi ya uzalishaji in-achangia kuletamabadiliko ya mapatokwa idadi kubwa yawafugaji kuku wadogo

wadogo katika jamii za vijijini. Ufanisihuo umethibitishwa na mpango waVECO katika wilaya ya Same,Kilimanjaro.

Mwaka 2007, Tanzania Veco iliun-ga mkono programu ya miaka mitanokuhusu usalama wa chakula katikawilaya za Simanjiro na Same kwalengo la kufanya kilimo ni shughuliyenye faida na manufaa kwa jamii zisi-zo na mazingira bora

Mpango huo ulirekebishwa mwa-ka 2008 na Veco katika mbinukuelekea kuimarisha usalama wachakula kwa familia za wakulima.

Mbinu ya SACD ,wote walihusikawa moja kwa moja katika shughuli zandani ya mnyororo wa bidhaa katikampangilio maalum.

Mbinu ya awali ya kilimo endelevukwa ajili ya usalama wa haikuchukuli-wa kwa uzityo mkubwa . Ilionekana nikwa ajili ya ustawi wa familia zawakulima 'kusababisha kuacha baadhiya masuala muhimu na vikwazo kuta-futiwa ufumbuzi..

Jinsi inavyofanya kaziMpango wa kuunga mkono

utekelezaji na makundi kupangwakatika kata nne za Kihurio, Makanyailiyopo, Maore na Same. Hii ilikuwamiaka mitatu wa mpango mkakati ku-saidia Wakulima Family ulioandaliwa(awamu ya pili) kuboresha maisha yao.

Veco, kupitia mdau wake wautekelezaji ( halmashauri ya wilayaSame), iliwezesha shirika na uimar-ishaji wa vikundi vya wakulima, kwakuimarishwa utoaji rahisi ya hudumaza ugani, mafunzo , uzoefu na kupun-guza gharama kwa kikundi.

Mafunzo yanayotolewea ni pamojana ufugaji bora, uzalishaji na usi-mamizi, masoko, kutunza kumbukum-bu, biashara ujuzi wa usimamizi,malezi ya kundi na uimarishaji wamakundi.

Mafunzo yanalenga kuwezeshwawakulima kufanya biashara na ku-boresha ubora na wingi wa kuku waasili. Pia kuboreshwa stadi za ujasiria-mali na uwezeshaji katika biashara yakuku.

Ujasiriamali miongoni mwa wafu-gaji kuku ukawa ni ujuzi mpya na njiaya maisha kwa ajili yao.

Wakulima si tu walipewa mafun-zo kwa uzalishaji na kuuza kuku, laki-ni mengi zaidi juu ya namna borawanaweza kuweka makampuni yaohai.

Wakulima wamekuwa wakitumia

stadi hizi ili kuboresha ustawi wa fa-milia zao na jamii kwa ujumla, na waokuendelea kuwekeza na kupanua bi-ashara zao.

Wajasiriamali walibadilishanawanunuzi na uzoefu mbalimbali .Wakulima wadogo wadogo sasawanawekeza katika mradi kuzalianaunaoonekana kuwa na faida zaidi.

Athari za muda mrefu.Athari za muda mrefu za kusaidia

kupangwa vikundi vya wakulimaumechangia thamani ya ziada ki-uchumi ni kwamba sehemu kubwa yaidadi ya watu maskini ni kupunguzaumaskini

. Baadhi ya mafanikio ni pamoja nakuwatumia kuku kibiashara, mradi wakilimo na kuboresha maisha ya watu.

Danstan Kihedu ni mkulimaanayeishi na mke na watoto wake

watatu katika kijiji cha Mpirani , kataya Maore , wilaya ya Same.

Amekuwa akiwatunza kuku tushughuli ya kujifurahisha tu tangumwaka 1998. Kama alivyosema, "Miminilikuwa natunza kuku tu kwa ajili yamahitaji ya mayai na nyama kwa ajiliya familia yangu.

"Nilikuwa nafuga kuku si zaidi yatano kwa wakati. Sikujua kwambakuku asili inaweza kubadilisha maishayangu kiuchumi. Ghafla, mradi wakuku umeboresha kabisa maisha yan-gu. Shukrani kwa mpango huu. "

Kihedu alijiunga na Muunganowa kundi mapema mwaka 2008.Kupitia kundi hili lililoingiliwa naVeco mpango katika kata ya Maore, al-ifanikiwa kuwabadilisha kuku wakekutoka wa kujikimu na kuwa katikakwa uzalishaji wa kibiashara.

Hii ilikuwa baada ya kupokea ma-funzo ya kiufundi kuhusu kilimo naufugaji wa biashara ya kuku kutokaBaraza la Wilaya ya Same. Alisemakuwa, kilimo cha biashara kimepanuamaarifa na ujuzi wake.

Kwa upande wa mapato yaKihedu yaliongezeka na akawa elimuya kutosha. Hatimaye akageuka kati-ka usambazaji wa vifaranga katika ki-jiji chake mwenyewe na vijiji jirani njeya kata ya Maore.

Soko kuu la vifaranga vyake niSame, Hedaru na Makanya. Anawezakuuza hadi vifaranga 400 kwa mpigo.Ana uwezo wa kuchanja vifarangakabla ya kuwauzia wateja wake nahivyo kufanya vifaranga wakewaaminike pamoja na vifaa wake."Mimi pia kuwapa ushauri wa jinsi yakuwatunza," aliongeza.

biashara amegeuza maisha yake.Yeye kujenga nyumba mbili naalikuwa na uwezo wa kulipa ada zashule kwa watoto wake. Kihedu anase-ma: "Kuku ni mali" maana kuku niutajiri.

Kupitia ujasiriamali, uzalishaji,mafunzo ya ujuzi na kibiashara yakuku, Danstan Kihedu amepanuamaarifa na ujuzi ambao umembadil-isha kutoka kujikimu na kuwa mkuli-ma wa kibiashara.

Pia, Shogholo ni mkulimaanayeishi na familia yake katika kataya Same wilayani Same. Alianza kufu-ga kuku mwishoni mwa mwaka 2008baada ya kujiunga na Umoja wakikundi chake. Alipata motisha baadaya kuona baadhi ya wanachamawaanzilishi wa kikundi hicho wakinu-faika na mafunzo na nyinginezo baada

ya Veco kuingilia mpango unaotolewakwa kundi.

Awali, hakuweza kushiriki katikakutunza kuku, kwa sababu alikuwabado mgeni katika mradi. Baada yakushiriki katika ziara ya mafunzohuko Mfiduo, alianza kufuga kuku 10.Polepole mradi ukaanza kupanukakwa kufuga vifaranga zaidi waloikuwawanazalishwa kutokana na usimamizibora na huduma. Yeye sasa anamilikihadi kuku 300 kwa wakati mmoja.

Anauza mayai, kuku na vifarangana kuboresha maisha. Anaweza kupa-ta hadi sh.350,000 kwa mwezi kamamapato kutokana na biashara hiyo.Kutokana na mapato hayo amewezakutatua mahitaji ya familia kama vileada ya shule, chakula na mahitajimengineyo.

Shogholo pia alijengwa nyumba ya

familia. Sasa ana mipango ya kupanuabiashara yake na kuwa na kundi kub-wa la kuku. Miongoni mwa faida zili-zopatikana kutoka kuingilia mpangokwamba kamwe hawezi kusahau ma-funzo ya kiufundi na ujuzi alioupatakuhusu uzalishaji wa kuku kibi-ashara.

Alisema, kwa njia ya mafunzombalimbali na Mfiduo, amepatamaarifa na ujuzi mwingi ambayoanaona kuna zaidi ya fedha. Maoniyake ni kwamba: "maarifa na ujuziuliopatikana ni mbegu kuelekeamafanikio ya kiuchumi na kijamii."

Magreth Mashambo ni mkulimaanayeishi katika wilaya ya Samemwenye watoto wake watano kati yaowasichana wawili na wavulanawatatu.

Alianza kufuga kuku baada ya mo-

tisha alioupata kupitia mpango huomwaka 2008. Awali, alikuwa akifugakuku kama chanzo cha mayai na nya-ma kwa familia yake.

Baadaye akaanza ufugaji wa kibi-ashara wa kuku asili na kuwa kuwachanzo kikuu cha mapato na kum-saidia mama moja; "Tumepanuka kib-iashara . Watoto hupata mahitaji yaoyote kutoka biashara hiyo. Biasharani kazi yangu. "

Mashambo ni miongoni mwawanachama waanzilishi wa kundi namkulima aitwaye Muungano. Kundililianzishwa mwaka 2008 kwa njia yauwezeshaji wa mpango Veco wilaya yaSame. Kundi lina wanachama 30,wanawake 25 na wanaume wa tano.

Kupitia mafunzo mbalimbali ya ki-ufundi kuhusu uzalishaji wa kukuwakibiashara, Mashambo imeweza

kuanzisha mradi wa kuku. Alianza nakuku 50.

Sasa ana makazi bora ya kisasakutokana na kuku.Alikuwaakichangia matofali ya ujenzi, maji nakazi wakati Veco imechangia saruji,bati na mbao za kujengea.

Ujenzi wa upanuzi wa makazikuimarishwa ya uzalishaji. Aliwezakuongeza idadi ya kuku hadi 150 ikiwani pamoja na baadhi ya majogooanaowakuza kwa miezi 3-4 kabla yakuuzwa kwa sh. 8000 kila mmoja.Anaweza kuendelea hadi majogoo 15wakati huo.

Kupitia mikopo midogo kutokaBenki ya Kijiji kundi lake na Jamii,limeweza kuendesha biashara vizuri.Hutoa vifaranga 50 kila mwezi.

"Mimi pia kuuza mayai. Nawezakupata hadi trei nne ya mayai kwamwezi. Trei kila kuuzwa katika sh.7500 kwa hiyo, mimi hupata 30,000kutokana na mayai. Vifaranga hu-uzwa sh 1000 kila mmoja. Mimi kupa-ta kiwango cha chini cha sh. 50,000 ku-toka biashara ya vifaranga "Anasemakwa wastani anaweza kulipwa hadish. 150,000 kwa mwezi.

" Ninawahudumia watoto wawiliwalio katika shule za sekondari, mvu-lana na msichana. Biashara hii ime-saidia sana tangu mume wangualiponiacha na watoto. Watoto hutege-mea kila kitu kutoka kwangu,"anaongeza.

Mume wa Mashambo kaendaMorogoro kuangalia ajira tangu mwa-ka 2007 na hajarudi nyuma. Licha yahadhi yake ya ndoa, Mashamboalikuwa na uwezo wa kutunza watotowake wawili wanaosoma shule yasekondari. Pia amekarabati nyumbayake.

11

A

VECOIjumaa Februari 22, 2013

10

A

VECOIjumaa Februari 22, 2013

Mpango kuboresha uhakika wa chakula, mabadiliko ya maisha

Tuma maoni yako bureukianza na neno INITIATIVEkwenda namba 15774

13

A

PROMOIjumaa Februari 22, 2013

12

A

BIASHARAIjumaa Februari 22, 2013

Na Majuka Ololkeri

Mengi yanasemwakuhusu kijana aumtu anayejihusishana kilimo. Wenginewanakiponda kilimona wakati mwingine

wana sababu zinazoweza zikakushaw-ishi kukubaliana nao. Tulifika Kilosana kuzungumza na vijana kuhusu kil-imo, soko lake, namna ya kujiendelezakatika kilimo na mengineyo.

Changamoto zinazowakabiliwakulima ni hizi

• Wakulima wengi wanalima bilakuwa na malengo

• Hakuna mfumo wa taarifa za ma-soko kuwawezesha wakulima ku-fahamu watauza wapi mazao yao

• Elimu ndogo juu ya uongezaji wathamani ya mazao wanayolimakama vile usindikaji

• Hakuna utunzaji mzuri wa mazao

• Kutojihusisha kwenye vikundi nataasisi za kifedha kama vile SAC-COS na VICOBA

• Kukosa uwezo wa kupanga bei yamazao

• Miundombinu ya barabara namawasiliano mbovu

• Ukosefu wa vyombo vya us-afirishaji kutoka maeneo ya uzal-ishaji

• Kutojua namna ya kutumia simuza mikononi kibiashara ili kupatataarifa

• Ubora wa mazao kupunguayanapofika sokoni

Madhara yake ni nini?

• Vijana wengi hukata tamaa ku-jishughulisha na kilimo kwa madaikwamba hakilipi

• Wakulima hukata tamaa kuen-deleza kilimo hata kuuza masham-ba

• Vijana kukimbilia mijini bila kuwana malengo

• Wengi hulima kwa ajili ya chakula

tu

Nini kifanyike?

• Sekta zinazohusika zitoe elimu yakilimo biashara ili wakulima wan-ufaike na kilimo

• Kuwe na msukumo wa matumiziya teknolojia sahihi za kilimokama vile kilimo cha umwagiliaji,mbegu sahihi kulingana na udongona hali ya hewa ya eneo lako.

• Wakulima wajifunze namna yakutafuta masoko na biashara juuya kilimo stahiki kinacholenga hi-taji la soko na walaji

• Kuwaunganisha wakulimakwenye masoko kwa kutumiateknolojia na mawasiliano mfanovipindi vya redio, simu za mkononina mengineyo.

• Kufanya tafiti za kuendeleza kil-imo biashara

• Miundombinu ya barabara, vy-ombo vya usafiri na mengineyoiboreshwe

• Elimu ya usindikaji itolewe kwawakulima

• Suala la kilimo biashara lipewekipaumbele katika ngazi zote iliwakulima waweze kuingia katikasoko la ushindani

• Huduma za pembejeo za kilimozisogee zaidi vijijini na ziwalengewakulima

SwaliJe ni changamoto zipi wanazoku-

tana nazo wakulima wa eneo lako?Unadhani nini kifanyike kutatuachangamoto hizo? Swali hili linaen-dana zaidi na makala hii.

Je, ni fursa zipi za kilimo biasharazinapatikana katika eneo lako?Unadhani zinakidhi mahitaji yawakulima?

Tuambie kwa kutumia mawasilianohapa chini;Barua pepe: [email protected]: 0715568222S.L.P. 2065, Dar es Salaam.

Kilimobiashara

ndiyo mpangomzima

15

A

MBEGUIjumaa Februari 22, 2013

14

A

MBEGUIjumaa Februari 22, 2013

Na Mwandishi Maalum, Ansaf

Serikali imepitisha sheriainayozuia wakulima kuch-agua, kutunza, na kubadil-ishana mbegu bora na fa-milia zao, marafiki na maji-rani; imefahamika.

Mabadiliko yaliyofanywa hivi karibunikatika mfumo wa kisheria kuhusuHaki Miliki juu ya mbegu na mimeambalimbali..

Wakati hali hii inaonekana kamasi muhimu sana na kuachiwa wanash-eria, inakuwa muhimu zaidi wakatiasilimia 70 ya wananchi wanategemeakilimo kwa maisha yao.

Mabadiliko hayo ni pamoja naSheria mpya ya Haki ya Mimea 2012,kusaini Mkataba wa Kimataifa juu yaAina ya Mimea (UPOV 1991), na utu-miaji wa mfumo wa kisheria kupitiauanachama wa Shirika la Hakimilikikanda ya Afrika (Aripo).

Mapendekezo ya mabadiliko yasheria zote tatu yataimarishaushirikiano wa kimataifa katika kud-hibiti mauzo ya mbegu duniani, na zai-di hasara kwa wakulima wadogo am-bao wanategemea mbegu kuwaokoakwa usalama wa chakula chao.

Serikali imekuwa ikisaidia sanaushiriki wa sekta binafsi katika kil-imo cha kisasa, na mfano kiasi kikub-wa cha kilimo cha kisasa na masham-ba makubwa kama muktadha wa kil-imo katika nchi unabadilika.

Jamii ya Biashara ya kimataifaimekuwa ikijihusisha na kuwekezakatika kilimo nchini Tanzania. Hiiinaleta njia mpya ya kufanya kazi nachangamoto, kampuni za kimataifa zambegu yanatafuta hakimiliki ya she-ria zilizo na mpya katika mimea ili ku-jitengenezea faida kupitia mauzo yambegu, dawa na mbolea.

Ajenda ya Mapinduzi mapya yakijani

Jamii ya Biashara ya kimataifaimekuwa ikijihusisha na kuwekezakatika kilimo nchini Tanzania. Hiiinaleta njia mpya ya kufanya kazi nachangamoto, kampuni za kimataifa zambegu zinatafuta hakimiliki ya sheriampya katika mimea ili kujitengenezeafaida kupitia mauzo ya mbegu, dawana mbolea.

Wapinzani wa ‘mapinduzi mapyaya kijani’ hawajaacha utekelezaji kati-ka kilimo, lakini wamewapa jukumumabingwa kusoma jinsi gani sheriakatika nchi za kiafrika zinawezakubadilishwa ili kuanzisha modelimpya ya kilimo. Wamebainisha kandaza biashara na mikata yaa kimataifakama sehemu ya kuanzia.

Nchi za kiafrika zinajipanga katikamakundi yakiwamo EAC, SADC, naComesa ni kama rutuba kwa ajili yakupanda sera ya mbegu na sheria zakanda kwa ajili ya kuunga mkonoutashi wa kampuni ya kimataifa.

Badala yake, wakulimawamekuwa wakifuatiliwa na ‘polisi wambegu’, mawakala wa kampuni kubwaambao kazi zao ni kuchunguza wakuli-ma na kuwapeleka kwenye sheria walewote wanaotunza mbegu.

Hapa katika Afrika zaidi ya asilim-ia 80 ya mauzo ya mbegu zinazozal-ishwa zinasambazwa bila ya utaratiburasmi,kutoka kwa mkulima kwendakwa mkulima. Wakulima wado-gowadogo katika Afrika Mashariki

wanatunza asilimia 60-70 ya mbegu zi-nazotumiwa shambani, wananunuaasilimia 30-40 ya mbegu zao kutokakwa ndugu na jirani na chini ya asilim-ia 10 per cent zinapatikana katika sek-ta rasmi kwa mfano kutoka kwawauzaji wa zana za kilimo.

Ukweli ni kwamba wakulimawadogo ni wazalishaji na watumiajiwakubwa wa mbegu katika Afrika nawamefanikiwa kulima na kuvunamazao kwa miongo mingi.

Mfumo wa mbegu wa mkulimakwa mkulima

Mfumo wa mbegu wa mkulimakwa mkulima unapunguza gharama zauzalishaji kwa kutunza uhuru kutokasekta ya biashara ya mbegu, wakatiubadilishanaji wa mbegu unahakik-isha mtiririko wa rasilimali, kuchangiamaendeleo ya mbegu sahihi za asili namazao kwa ujumla. Tunahitaji kuungamkono maendeleo ya mfumo huu, am-bao ni rasilimali muhimu kwa kilimocha kisasa na cha asili.

Kuna utambuzi mpana waumuhimu wa mfumo wa wakulimawadogowadogo kumudu mbegu na fur-sa muhimu kwa wanawake kuen-deleza. Kwa hifadhi ya mbegu zashambani zinatambuliwa katikamikataba ya kimataifa kama vile theInternational Treaty on Plant GeneticResources (ITPGRFA) na theConvention on Biological Diversity(CBD).

Tanzania imetia saini kuridhiamikataba yote miwili , lakini inashind-wa kutambua mchango wa wakulimana haki zao katika kushiriki au kun-ufaika na faida katika wimbi jipya lasheria mpya iliyotiwa saini.

Sheria ya The Plant BreedersRights Bill 2012 imepitishwa kuwasheria za Tanzania. Zitatumikakuimarisha haki za sekta ya biasharaya mbegu na kuwabana jamii yawakulima, na kuathiri maisha ya watuwengi na usalama wa chakula kwawakulima wadogo wa Tanzania.

Sehria hiyo inatoa haki ya kuuzambegu kwa wale wanaoanzisha ainampya. Kwa kina inaruhusu tu wakuli-ma kutumia “ mbegu zilizovunwa (ku-patikana katika mimea yao) kwa ajiliya dhamira ya propaganda katika hi-maya yao”.

Hii inamaanisha kuwa wakulimahawawezi kutunza, kubadilisha na ku-uza mbegu kutoka katika aina zili-zozuiwa. Kwa mfano katika modeli yaMapinduzi ya kijani, kampuni za mbe-gu za kimataifa zimmetumawanasayansi wake nchini Tanzania ilikuendeleza mbegu zilizoboreshwa.Wanachukua mbegu za asili zinazoen-delea kuwapo licha ya mazingiramagumu na kuziboresha kwakuzichanganya na nyinginezo au kwakuanzisha aina nyingine ya kufaniki-wa.

Kisha wanazisajiri kama ainampya ya mbegu chini ya Sheria nakisha kuwa na haki pekee za kuuzambegu hizo kwa miaka 25-30. Kamamkulima anataka kutumia mbegu hizoanatakiwa kuzinunua kutoka kwenyekampuni za mbegu. Kama mimea,hatakiwi kutunza mbegu zilizovunwakwa namna yoyote ile zaidi ya matu-mizi yake.

Hawezi kutoa au kubadilishanabaadhi na jirani na hawezi kuuza kwanamna yoyote ile. Pia mazao ya mbegu

hizo zilizoboreshwa zinapoteza uasiliwa wazazi wake na hivyo mbegu zi-nakuwa hazina maana.

Kununua mbegu mwaka hadimwaka

Sasa wakulima wanalazimika ku-nunua mbegu mwaka hadi mwaka ku-toka kwa wauzaji wa zana za kilimo,ambao wanawahimiza kuongezambolea na dawa ambazo wanaziuza.

Na hakuna utambuzi kwa jukumula wakulima katika uendelezaji wambegu zilizopo. Hazina ya akiba yambegu katika sekta isiyo rasmiinatekelezwa na hivyo mbegu pekee zi-nazopatikana ni aghali kuzinunua.

Fursa mbadala katika suala hili nikwa wakulima kufanya kazi nawafanyakazi wa nchini na taasisi zakilimo za utafiti kufanya majaribio,kuchagua na kuzalisha zaidi mbegubora na kuzisajiri na Tanzania OfficialSeed Certification Institute (TOSCI),na kisha kuwa na uwezo wa kubadilis-hana na kuuza mbegu kwa wakulimana vijiji vya jirani, ambao wanatambuambegu hizi kuwa zina ubora wa hali yajuu, na watafanikiwa katika mazingiraya nchi yao.

Bei zitakuwa chini, na wakulimawa nchini (wanaume na wanawake)watakuwa na udhibiti kwa mbegu zaona chakula, huku wakirutubishabionuwai ambayo Tabnzania imekuwaikifurahia (Tanzania ni nchi ya 11kwa kuwa na bionuwai bora zaididunia).

Haki ya kumiliki itabakia kuwamali ya umma. NJia hii tayari in-afanya kazi katika baadhi ya maeneoya Tanzania, na hadi sasa imekuwa ik-itiwa nguvu na serikali chini ya mfumoujulikanao the Quality Declared Seedsystem. Kama mbegu hizo zitasajiriwachini ya sheria mpya( PBR Bill) zoezihili litafanikiwa.

Mabingwa wa mbegu dunianiKwa mujibu wa kundi linalojiende-

sha bila ya faida- ETC Group, wazal-ishaji sita wakubwa wa zana za kilimo,ambao wanamiliki karibu asilimia 75ya soko la dawa za wadudu na mimeaduniani ndiyo mabingwa wanaoshikil-ia sekta ya mbegu. Monsanto, kampunikubwa zaidi ya mbegu ni ya tano kwauzalishaji wa zana za kilimo. Syngenta,kampuni ya pili kwa ukubwa ya zanaza kilimo pia ni kampuni ya tatu kwauzalishaji mbegu duniani.

Bayer, kampuni kubwa ya uzal-ishaji wa zana za kilimo pia ni kam-puni ya saba kwa uzalishaji wa mbegu.Na DuPont, kampuni kubwa ya pilidunia ya uzalishaji wa mbegu pia nikampuni ya sita kwa uzalishaji wazana za kilimo. Kampuni zina-jishughulisha kusafirisha nje duniani

na yanaungwa mkono na serikali zaoambayo yanahitaji mapato kwa ajili yakurekebisha nakisi zao.

Faida nyingine ni wawekezajiwakubwa duniani ambao wanachangiakatika kukabiliana na ongezeko la beiya chakula, ongezeko la nyama (kul-isha wanyama) kwa ongezeko la ghaflala daraja la kati la uchumi, nakuhamia kutoka kwa matumizi ya gesiukaa na matumizi ya nishati ya mafu-ta ya mimea. Uwekezaji huo mkubwawa mabilioni ya dola yamekuwa yaki-fadhili miradi mkubwa ya mashambakatika ardhi ambazo ni bei rahisi – nahawapati sehemu nyingine kwa beirahisi kama Tanzania.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifawa Kuhusu Haki ya Chakula, Olivierde Schutter, anatahadharisha “utaala-mu wa kupandikiza mbegu na kuten-ganishwa katika kilimo unaongozakatika hatua za haraka za mfumo wabiashara wa mbegu, pamoja na mfumowa mbegu wa wakulima kuitia kwawakulima wa jadi unatunza, kubadil-isha na kuuza mbegu katika mfumousio rasmi”

Faida za ukiritimbaKuhama huku unatoa fursa za

muda kwa wapandaji wa mimea nahaki miliki kuitia Haki miliki, kamanjia za kuhimiza utafiti na upandikiza-ji wa mimea. Katika mchakato huu,hata hivyo wakulima maskini wataen-delea kuwa tegemezi katika pembejeoza bei mbaya, kujihatarisha katikamadeni makubwa na kujikuta katikamapato yasiyotengemaa.

Utafiti unaoongozwa na sekta bi-nafsi unaweza kutosheleza nmahitajiya wakulima na katika nchi zilizoende-lea na kuwapuuzia wale wakulimamaskini waliopo katika nchi zilizoende-lea.

Mfumo wa mbegu kwa wakulimawanawezakujikuta katika changamotolicha ya kwamba wakulima wengi kati-ka nchi zilizoendelea bado wanatege-mea katika mfumo huo licha ya kuwawakulima wengi katika nchi zilizoen-delea bado wanategemea katika mfu-mo huo ambao kwao ni chanzo chauhuru wa uchumi na tegemeo kwatishio kama la wadudu, magonjwa namabadiliko ya tabia nchi.

Kwa ujumla, zana za kilimo zi-naweza kutishiwa na kutiwa moyo ma-suala ya biashara ya aina mbalimbali.Wakulima, wakiwamo wakulimawanawake, wanahitaji haki halisi ku-toka kwa watunga sera na wenyedhama ya maamuzi?

Je kwa nini Tanzania imetiasaini?

Sasa ni muhimu kutambua kwanini Tanzania imetia saini mkataba wakimataifa (UPOV 1991) ambao unalin-da haki za kampuni za kimataifa zina-zojishushulisha na zana za kilimo nakudhoofisha haki za wakulima.

Hivi karibuni, Tanzania ilijiungana the International Union for theProtection of New Varieties of Plants(UPOV 1991). Sasa ni nchi ya piliKusini ya jangwa la Sahara Afrika ku-fanya hivyo baada ya Afrika Kusini.

Mawakala huru wamekuwawakipiga kelele kutahadharishakuhusu kujiunga na UPOV. Grain,kama taasisi ya kimataifa isiyozalishafaida inayofanya kazi ya kuungamkono wakulima wadogo wadogo kati-

Wakulima wazuiwa kutunza na kubadilishana mbegu bora

“Utafitiunaoongozwa nasekta binafsiunawezakutoshelezanmahitaji yawakulima...

ka mapambano yao dhidi jamii zina-zoathiriwa na mfumo usiozingatiabionuwai inasema kuwa:

“UPOV inapuuzia haki za wakuli-ma. Haki ya uhuru wao wa kutunzambegu kutokana na mavuno yao.Katika maana pana ni kwamba, UPOVhaitambui wala kuunga mkono haki zajamii kwa bionuwai na nafasi yao yakutekeleza. “Kampuni za nchi zaKaskazini zitachukua mfumo wa taifawa mbegu katika nchi za Kusini.Kampuni za taifa na kampuni za waza-lishaji wengine wa mbegu zitanunuli-wa na kampuni za nje. Kampuni zaKaskazini zitapata haki ya bionuwaiya Kusini bila ya kujali kugawana fai-da.

“UPOV haitoi fursa kwa faidakushirikiana kutoka Kaskazini kwabaionuwai ya Kusini. Wakulima wakusini watajikuta wakilipwa tu mira-haba kwa ajili ya mali zao ambazozimechakachukuliwa na kupangwaupya na Kaskazini.”

“ Kigezo cha UPOV kwa ulinzi ki-tachangia mmomonyoko wabaionuwai. Hii itachangia kushushamavuno na kusababisha usalama mdo-go wa chakula. Kujiunga na UPOVmaana yake ni kwamba kushiriki kati-ka mfumo ambao unaunga mkono hakiza wenye viwanda wakubwa na kukan-damiza wakulima.

“UPOV imeundwa kufanikishaukiritimba katika uzalishaji wa mbe-gu. Licha ya miaka 35 ya Mapinduziya Kijani na UPOV, ya Kusini pamojahakuna usalama wa chakula.Kujiunga na mfumo kama UPOV uta-hakikisha kuwa Kaskazini inamilikimfumo wa masoko yanayoongezekalakini si kwa faida ya nchi ambazo zinanjaa sasa.” Graham Dutfield, Profesawa Utawala wa Bora Kimataifa katikachuo kikuu –‘Leeds University Schoolof Law’, anasema , “wachambuziwanachambua mfumo wa UPOVkwamba haufai kwa kilimo katika nchizinazoendelea.”

Lakini UPOV inafaa kuendelezamfumo wa viwanda na kuunga mkonosekta ya mbegu ya kibiashara (iki-wamo kuendeleza kilimo kwa pembe-jeo za viwandani) dhidi ya wakulimawadogo na maarifa ya jadi.

Mkazo katika sekta ya mbeguWengi wanatilia mkazo katika sek-

ta ya mbegu kwa karibu miongo mi-wili, wakisema kwamba mkazo huoukiwamo Hakimiliki ya kulingana naulinzi wa hakimiliki na ulinzi wa mbe-gu haiendi sambamba na haki za bi-nadamu. Wachambuzi wanasemakuwa uboreshaji wa mavuno tanguUPOV ilipoanza kufanya kazi unatoakipaumbele zaidi kwa maendeleo yasayansi kuliko ulinzi wa hakimiliki nakwa hiyo hii inakwenda sambamba nakupotea kwa bionuwai.

Mfumo wa UPOV hautambuimchango wa mkulima kwa miongokwa ajili ya maendeleo ya mazaomapya, na kwamba maendeleo yamazao na uboreshaji umetokea tangukilimo kianze hata kabla ya kuwapokwa hakimiliki.

Dutfield ametahadharisha,“Inavyoonekana ni kuwa idadi ya nchizinazoendelea zinajiunga na UPOVkwa sababu za kisiasa na msukumowa kiuchumi, bila ya kufikiria kwamakini kama uanachama wa UPOVutachangia kwa muda mrefu katika

sera za nchi katika maeneo muhimukatika maeneo muhimu yakiwamo yamaendeleo ya uchumi, usalama wachakula na bionuwai.”

Rasimu ya Aripo ni jaribu jingineya kuhusisha UPOV 91 katika nchi 14za Afrika, ikiwamo Tanzania. Mfumowa sheria hautoi fursa kwa maendeleomuhimu yanayofaa kwa kutekelezamahitaji ya kikanda. Ni kiasi chakulinda sekta binafsi kwa maslahi yawakulima wadogo.

Mfumo huu wa kisheria , kamaukitekelezwa utaifunga Tanzania kwaUPOV 91 na aina yoyote ye sheria yanchi itafanyakazi kwa kuzingatiamazingira hayo.

Kuhamia kwa kilimo-viwandaKwa pamoja, mabadiliko ya sheria

hizo tatu yanatoa fursa kwa njia yakuhama kuelekea kwenye viwandavya kilimo, na kufanya kampuni kub-wa kutekeleza maslahi ya wadauwenye hisa, lakini wawajibika kidogokwa mahitaji ya mamilioni ya wakuli-ma wadogo ambao wanategemea mfu-mo wa mbegu kwa maisha yao.

Kinachovutia ni kwamba, Umojawa Afrika (AU) umetoa modeli ya she-ria kwa masuala haya, ambayo yana-toa usalama kwa wakulima wadogo nakutambua nafasi yao muhimu katikakulinda bionuwai na maendeleo yambegu.

Wanaoandaa rasimu mpyawamepuuzia ushauri wa AU na kuonakuwa wanazingatia sana suala la hakiza wenye viwanda. Modeli ya AUinatilia mkazo hakimiliki dhidi yamaarifa ya jadi na kuzuia hakimiliki zamaisha yote na mchakato wa kibiolojia.Pia unalinda haki za wakulima kutun-za, kutumia, kubadilishana na kuuzambegu zao.

Mapendekezo ya fursa sawaKwa hiyo, hapa kuna mapendeke-

zo machache ya kusaidia kuwekauwanja sawa ikiwamo kutazama upyarasimu hiyo- Plant Breeders RightsBill, na kuubadilisha na mwingine un-azozingatia modeli ya AU-AfricanUnion Model Law – ambao unatoauwiano sawa na umuhimu wa kulindakampuni za mbegu ikiwamo mahitajiya kulinda haki za wakulima.

Kuchelewesha kujiunga na UPOV1991 hadi sekta ya kilimo ya Tanzaniainaendelezwa katika nafasi ambayotaifa litanufaika kutokana na UPOVna kuanza kusikiliza sauti za huruwanasayansi huru wa dunia, Umojawa Mataifa na AU, wanaopinga kilimokwa ajili ya kilimo cha viwanda na ku-unga mkono ikolojia ya kilimo.

Pia inapendekeza kupanua ukwelikwamba sheria hii inashinikizwa nakampuni za zana za kilimo za ki-mataifa na wawekezaji ambao wanata-ka kutumia fursa ya uwekezaji katikaeneo ambalo kwa sasa linahitajikasana duniani. Kilimo cha Afrika.

Mwisho kabisa ni kwamba , inaju-muisha kundi la wakulima waTanzania kikamilifu katika maendeleoya sheria kuhakikisha kuwainatekeleza hasa mahitaji ya jamii yawakulima,watu ambao wanalishataifa.

Tuma maoni yako bureukianza na neno SEEDSkwenda namba 15774

16

A

SAFUIjumaa Februari 22, 2013

KUNA hatari nyingi zina-zoyakabili maisha kati-ka dunia hii. Wataalamwameainisha vitishosita vikubwa zaidi kati-ka zama zetu yaani

mabadiliko ya tabia nchi, uhaba wamaji, uhaba wa chakula, baharikuchemka, ukataji wa misitu naupotevu wa bionuwai.

Ingawa vitisho hivi vinaweza kus-ababisha madhara. Uwapo wake un-aweza kusababisha madhara makub-wa kwa dunia hii na kupoteza maishakatika sayari.

Leo hii, hebu tujadili kuhusu idadi.Hesabu inaweza sana kuvutia marakwa mara, lakini si mara zote waowatakuachia tabasamu usoni na hiiitakuwa moja ya nyakati hizo.Mabadiliko ya tabianchi ni sualalinalojitokeza sana katika jitihada za

kukabiliana na hali hiyo na juhudikubwa zimekuwa zikichukuliwa kati-ka kukabiliana nayo.

Je, unajua kwamba moja yasababu ya msingi ya mabadiliko ya haliya hewa ni ufugaji wa mifugo? Karibuasilimia 51 ya uzalishaji wa binadamuunaosababisha kuzalisha gesi chafu zi-naelekezwa kwenye mifugo na mazaoyake. Sekta ya ufugaji ni chanzo kikuucha uzalishaji wa hewa ukaa na nitro-jeni ambayo ni mara 300 zaidi kulikohewa ukaa (kaboni dioksidi).

Ufugaji wa mifugo pia ni sababuya kuwapo mgogoro wa chakula.Karibu nusu ya nafaka inayozalishwaduniani hutumiwa kwa ajili ya malishona kunenepesha mifugo. Hii ni kwagharama ya watoto milioni 11 dunianikote katika nchi zinazozalisha nafakahizi; ambao hufa kutokana na njaa kilamwaka.

Wanasayansi wanasema kuwakupunguza mifugo kutasaidia kuweze-sha nafaka hizo ziweze kutolewa kwawatu kukabiliana na ongezeko la ida-di ya watu na hivyo kuondokana namgogoro wa chakula.

Kuna mambo mengi ambayohuchangia mgogoro huu wa chakula,ambao tayari ni wa kutisha katikanchi maskini na tishio kwa matajiri.Moja ya kashfa ya mfumo wetu wachakula duniani ni kwamba karibuwatu bilioni moja wanakabiliwa nanjaa na utapiamlo.

Wanyama karibu bilioni 67 kwamwaka wanatumiwa kwa ajili yamaziwa ya unga, na mayai. Ufugaji nikuwajibika kwa asilimia 18 kimataifakatika uzalishaji wa gesi chafu am-bayo huchangia katika mabadiliko yahali ya hewa ya hatari. Zaidi ya asilim-ia 30 ya nafaka kimataifa ikiwa nipamoja na ngano na mahindi na asil-imia 90 ya soya hutumiwa kulishamifugo. Kuzalisha kilo moja ya nyamaya aina ya nyama, kilo kumi ya mal-isho ya wanyama ni kutumia kilo tanoza nafaka kuzalisha kilo moja ya nya-ma ya nguruwe na kilo tatu ya nafakakuzalisha kilo moja ya chakula chakuku.

Sasa, umri wa wastani wa ng'ombealiyekua vizuri na kufikia uzito wa kilo300, hii itahitaji kilo 3000 ya malishoya wanyama kwa mazao hayo.

Kama mkulima mwenye mifugoalikuwa na mifugo 100, alitumia kilo300,000 za nafaka kulisha wanyama.Kisha jiulize tena jinsi watoto wengina kwamba kama kiasi hicho wangepe-

wa watoto wakala kwa sababu baadaya ng'ombe kuchinjwa nyama inakuwaghali kuinunua kwa ajili ya watu wen-gi na kujikuta haiwanufaishi watumaskini.

Moja kwa moja nafaka zinawezakulisha idadi ya watu wote wa duniakwa urahisi. Ufumbuzi mwinginerahisi kusaidia kurekebisha hali hii nikwa ajili ya wakazi kupunguza ulajiwa jumla wa nyama na maziwa, nakuchagua bidhaa za wanyama tu kuto-ka mifumo ya juu ya ustawi ambayohulipwa zaidi kuhusu ulinzi wa mazin-gira na ustawi wa wanyama.

Ripoti ya programu ya Umoja waMataifa ya Mazingira ya Juni 2010 naTume ya Ulaya ilihitimisha kwambapunguzo kubwa la athari za mazingirainawezekana kwa mabadiliko makub-wa duniani kote ya chakula na bidhaaza wanyama wote.

Kila mtu lazima kutoa kipaumbelekwa sehemu yake katika kupambanana mabadiliko ya tabianchi naongezeko la joto duniani. Kipaumbeleisiwe tu kwa sifa ya kiuchumi au kisi-asa wa mataifa kwa mtu binafsi au sisikuweza kupoteza maisha yote juu yasayari yetu; binadamu, wanyama,mimea, miti na mengineyo.

"Kama wanadamu, sisi ni hatarikuwachanganya mno na kutokutabiri-ka. Katika uzoefu wetu wa kila siku,kama kitu fulani hakijawahi kutokeakabla, sisi ni salama katika kuchukuahatua na haitaweza kutokea katikasiku zijazo, lakini isipokuwa inawezakukua wewe na mabadiliko ya tabianchi, " anasema Al Gore.

Tatizo la ufugaji wanyamana mabadiliko ya tabia nchi

KILIMOKWANZADIRECTORY

WATER AND SANITATION

Dar es Salaam Water and Sewerage Authority(DAWASA) – Tel: +255 22 276 0006

Dar es Salaam Water and Sewarage Corporation(DAWASCO) Tel: +255 22-2131191/4

Drilling and Dam Construction Agency (DDCA)Tel: +255 22 2410430/2410299

Energy and Water Utilities Regulatory Authority Tel: +255 22 2123850, 22 2123853

Ministry of WaterTel: +255 22 245 1448

INDUSTRY SUPPORT AND ASSOCIATIONS

Small Industries Development Organization(SIDO) – Email: [email protected], [email protected]

Agricultural Non State Actors Forum,P.O Box 33562, Dar es Salaam,TEL: + 255 22 2771566 / 2775970

Agricultural Council of TanzaniaTel: 255 22 2124851

CNFA - [email protected]

TCCIA Iringa Regional Chamber Tel: +255 26 2702486.

Tractors Limited Cells: +255 784 421606, 786 150213

Export Processing Zones in Tanzania (EPZ)Tel: +255 22 2451827-9

Agricultural Economics Society of Tanzania(AGREST) – Tel. +255-23 260 3415

Tanzania National Business Council (TNBC)Tel: +255 22 2122984-6

Tanzania Agriculture Partnership (TAP)Tel: +255 22 2124851

Tanzania Milk Processors Association (TAMPA)Tel: +255 222 450 426

Rural Livelihood Development Company (RLDC)Tel: +255 26 2321455

Tanzania Cotton BoardTel: +255 22 2122564, 2128347

AGRO-PROCESSING

TANEXA, Samora Avenue, N.I.C InvestmentHouse 6th Floor, Wing A, P. O BOX 1175 Dar es Salaam Tanzania [email protected], www.tanexa.com Tel:+255-732-924564 Fax: +255-22-2125432

ERTH Food - Tel: +255 22 2862040

Tanzania Organic Agriculture MovementPO Box 70089 DSM. Tel: 0732975739

ASAS Diaries Limited - Tel: +255 26 2725200

Tanga Fresh – Tel +255 27 2644238

NatureRipe Kilimanjaro LimitedTel: +255 22 21 51457

EQUIPMENT

Gurudumu Tatu LimitedTel: +255 22 2865632 / 2863699

National Service Corporation Sole (SUMAJKT)Cell: +255 717 993 874, 715 787 887

FINANCE

Private Agricultural Sector Support (PASS)Tel: 023-3752/3758/3765

Community Bank AssociationTel: +255 22 2123245

AGRO-INPUTS

Minjingu Mines & Fertilizers LtdTel: +255 27 253 9259 250 4679

KwetuAfrika

Na Nicolas

Begisen

www.best-ac.org www.ansaf.or.tzImefadhiliwa na